Mlinzi wa kimasai ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja anayelinda eneo la Retco bar mjini Iringa akiwa amepoteza fahamu kando kando ya barabara ya Iringa-Dodoma leo majira ya saa 2 hivi usiku baada ya kudaiwa kunywa pombe za ofa kupita kiasi katika bar moja iliyopo eneo hiloWalinzi wenzake katika eneo hilo wakijaribu kumwamsha pasipo mafanikio kwa zaidi ya masaa matatu akiwa amelala eneo hilo bila kujitambua huku akiwa na begi lake pembeni ,begi ambalo hata hivyo lilisachiwa vilivyo na vijana wa mitaani ambao walikutwa eneo hiloHapa wakijaribu kumnyanyua ila bado mlinzi huyo alikuwa hajiwezi na kuwa ndembe ndembe. Ama hakika...Chonde chonde! Ulevi noma....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. SASA HAPA WABAKAJI WAKIMBAKA ITAKUWAJE JAMANI.NA KAZI HAPO SIJUI ITAFANYIKA VIPI NA WAKIFUKUZWA KAZI WANALALAMIKA.

    ReplyDelete
  2. YOTE HAYO NI MAISHA; HUYO JAMAA MIMI SIMJUI, lakini ningependa kusema tu kwamba sidhani kwamba hiyo ndio tabia yake ya kila siku. Pombe ina sifa zake, mojawapo ni kwamba haina mbabe wala mtemi; pombe inamfanyia mtu yoyote kwa kiwango chochote; inategemea tu na pombe yenyewe on that particular day. Pombe kama vitu chengine chochote; haipaswi kutumiwa kupita kiasi; na inashauriwa kuiepuka kwa wasio weza kuistahamilia

    ReplyDelete
  3. mmbu imetafuna mimi....kama shamba

    ReplyDelete
  4. Wewe mdau uliyeleta lile tangazo la Masai waliolewa, nilivyoona hii tu nikakumbuka na kucheka sana. Kumbe ile ni kweli eeeeeeh.

    Hapo kama ni kibarua cha private itakuwa kimekwenda na maji.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...