Na Mwandishi wetu Marekani
Watu kutoka Canada na miji mbalimbali ya Marekani wanatarajiwa kufurika katika mji wa College Park, Maryland, ambao uko karibu na jiji la ofisi za kiserikali la Washington DC. Akiwa Marekani anatarajiwa kutembelea miji mbalimbali ikiwemo Houston na Dallas huko Texas. Wenyeji wake huko College Park, Maryland ndiyo wana ratiba kamili ya safari hizi. 

Mwandishi amewasiliana na mmoja wa viongozi wenyeji na wako tayari kuupokea ugeni toka Tanzania na sehemu mbalimbali kwa wiki hiyo ya tarehe 3-9 Oktoba ambayo matendo makubwa ya Mungu yanatarajiwa kutendeka. 

Semina na Conference hii itaongelea mada mbalimbali na kuendeshwa na watumishi wa Mungu wakiwemo kutoka Tanzania na Marekani. Kwa habari zaidi na kwa wale wanaopenda kuhudhuria; tafadhali tembelea hapa: http://thewayofthecrossgospelministries.org/upcoming-events-page.

Wenyeji wanakutarajia ufike ili upokee na kama hutaweza basi jitahidi kuiombea huduma hii na Mungu awabariki sana. Tunawatakia wote waalikwa na wenyeji baraka za Mungu.
Christina Shusho
 Kila mtu ana kitu alichokabidhiwa na Mungu (assignment) kuja kukifanya hapa duniani kwa ajili ya jumuia. Utajuaje kama unachoendelea kufanya ndicho ulichoitiwa kufanya? Mara nyingi utaona unafurahia unapokifanya na watu wanabarikiwa wanapohudumiwa kama kitu hicho kinahusisha huduma kwa jamii.
 Wengi mtakubaliana nami kwamba Christina Shusho amebarikiwa kuwahudumia watu kwa njia ya uimbaji wa nyimbo za injili. Huduma yake inabariki watu wengi sana na anapohudumia kwenye mikutano; watu wengi huhudhuria ili wasikose baraka zao. Nyimbo zake zina jumbe zinazogusa watu na mambo wanayopitia. Mungu amemwinua na anazidi kumtumia. Hivi karibuni Shusho alitunukiwa tuzo na East African Music Awards (EAMA’S) iliyofanyika mjini Nairobi Kenya kupitia wimbo wake maarufu ‘Unikumbuke’. Kwa hili wote tunampongeza sana na kumtakia mafanikio zaidi kwa kazi ya kuitangaza injili .


 Christina ni mtungaji wa nyimbo zake na utakubaliana nami kwamba Mungu amempa kipaji cha kuongea na mioyo ya watu. Nyimbo zake zimeleta faraja, upendo, amani, uponyaji, n.k. Siri kubwa ninayoiona katika utungaji wake ni kwamba huimba neno la Mungu. Kwa mwaka huu wa 2011 ametoa albam mbili ambazo bado ziko kwenye sauti (Audio): ‘Nipe macho’ na ‘Kwa kanisa la Mungu’. Albam zote ni nzuri na zimeongeza kuwabariki watu sana. Habari tulizo nazo ni kwamba video zinapikwa na zitakuwa sokoni wakati wowote kabla ya mwisho wa mwaka.

 Huduma ya Christina inaendelea kuvuka mipaka ya Tanzania; mpaka sasa ameshahudumia nchi nyingi za nje ikiwa ni pamoja na Kenya, Congo (DRC), Uingereza na Afrika ya Kusini. Kualikwa kwake hivi karibuni huko Marekani katika mji wa College Park Maryland ni neema ileile ya Mungu ya kuendelea kuipanua huduma yake. Tunaamini Mungu atatenda mambo makubwa na watu watabarikiwa sana.


Christina akishukuru kwa ajili ya tuzo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...