Boda boda yenye nambari za usajili T 592 BAZ ikiwa iko chini mara baada ya kusababisha ajali mbaya sana iliyopelekea kufariki dunia papo hapo kwa dereva wa bodaboda hiyo mara baada ra kugongwa na gari aina ya Land Cruser VX lenye nambari za usajili T 101 BGW leo maeneo ya kijiji cha Mandera nje kidogo ya mji wa Chalinze mkoani Pwani.ajali hiyo imetokea mapema lea asubuhi baada ya bodaboda hiyo kuingia kwenye barabara kubwa bila ya kuwa na tahadhali,ambapo dereva wa gari hilo lililokuwa likitokea Segera kuelekea Dar alijaribu kuikwepa bodaboda hiyo bila mafanikio na hatimae gari hilo likapinduka mara tatu na kuingia kichakani kama inavyoonekana pichani.watu waliokuwepo kwenye gari hilo wametoka salama ila ni dereva wa pikipiki (bodaboda) hiyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja ndie aliefariki dunia.
Gari ikiwa kichakani mara baada ya kupinduka mara tatu kutokana na kujaribu kuikwepa boda boda iliyoingia barabarani ghafla na kupelekea kuigonga na kusababisha kifo cha dereva wa pikipiki hiyo.
Askari wa Usalama Barabarani akiikagua gari hiyo.
Mashuhuda waliokuwepo wakati ajali hiyo inatokea.






Asa we mbwiga uliyetoa comment ya kwanza hapo juu ndo unataka kusema nini? Kuwa hao mabwana zako wazungu ndo kwao hakunaga ajali? Unajua maana ya ajali wewe?
ReplyDeleteAjali nyingi za Tanzania si ajali.. ni makusudi. Kama unaingia barabarani bila kuangalia unategemea nini? Umeona tena hiyo ya Morogoro? Mdau wa kwanza kwa kiasi flani yuko sahihi.
ReplyDeletekuna mjingamjinga mmija katoa maoni hapo juu, huyo wa kwanza, nashauri akapelekwe Mirembe. Anaposema Africans are stupid, yeye ni nani? Kwa uhakika huyu nae ni mwafrika, hivyo nae ni mpumbavu pia, anajitukana. Hawa ndio wale watu wanaofikiri kuwa Wazungu na Ulaya yao huwa hawana mambo mabaya. Hivyo ninamshauri kama hana cha kuongea, ni vyema akakaa kimya bila kutoa comments zozote. wajinga kama hawa wasipewe nafasi katika blogu yenye heshima kama hii jamani.
ReplyDeletewewe any 08:42 ndio upelekwe milembe wewe pamoja na hao wanaotoa leseni za pikipiki kubeba abiria then tembea uone mipango mizuri ya wenzetu au mpaka afe babu yako ndio ujue ajali nyingi za bongo ni uzembe sio bahati mbaya! only TAX and UDA nothing else
ReplyDelete