Kwa niaba ya kamati ya maandalizi ya dua kwa waliofariki kutokana na ajali ya kuzama kwa Meli Zanzibar. Uongozi wa kamati hiyo ya Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Kimataifa (International Isalmic University Malaysia) campus ya Gombak unapenda kutoa shukrani za
dhati:

Kwanza, kutokana na michango iliyopekea kufanyika dua hiyo kwa utaratibu mzuri.

Pili, tunawashukuru wanafunzi wa Tanzania wanaosoma vyuo mbali mbali nchini Malaysia, kwa kuhudhuria kwao kwa wingi. Ni wazi kufika kwao ni ishara ya mashirikiano mazuri yaliyoibua hisia za udugu, upendo na umoja kama ni watu wa taifa moja, zaidi mahudhurio yao yamethibitisha kujali ukubwa wa msiba uliogusa nafisi za wengi kwa kuwaombea dua waliofariki.

Allah (S. W) awape subira waathirika na msiba huu na azikubali dua zetu, 
Aaamin.
Ahsante

Rashid A. Mukki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...