Pili ni pale kaka Ndesanjo Macha aliponitahadharisha kwamba ukianza kublog ni sawa na kujiambukiza ugonjwa usiotibika. Yaani mtu unakuwa kama umeehuka na hufikilii jambo linguine zaidi ya kublog. Macho kumchuzi yakaja tena. Ilikuwa ngumu kumuamini kwamba haka ‘kaugonjwa ka kublog’ kakikuingia mwilini hakatoki. Sasa naamini maneno yake maana haipiti dakika bila kuwaza niwatumikie vipi wadau.
Tatu ni pale kaka Ndensanjo Macha aliponitahadharisha kuhusu comment moderation. Yaani hii ya kupitia maoni yote yanayotumwa na kuchuja yanayofaa kusomeka na yasiyofaa, kwa mujibu wa sera za blogu yako. Macho kumchuzi yakaja tena. Safari hii ni kwa sababu wakati huo sikuwahi kuwaza kwamba kuna wadau ambao kazi yao ni kutukana, kujeruhi hisia za watu na kuchafua hali ya hewa. Hakika sikuwa nimemuelewa hadi baada ya kuanza kupitia maoni takriban 3000 kwa siku. Nashukuru kwamba kazi hiyo, yenye lawama tele kutokana na baadhi ya wadau wachache kutaka kutema cheche zao kupitia Globu ya Jamii kujikuta wakikwama, wakisahau kwamba sera ya Globu ya Jamii iliyotanabaishwa kila unapotaka kutuma maoni ya 'Angalia usijeruhi hisia za mtu/watu' inabakia pale pale kwa nia njema hiyo hiyo, na si vinginevyo.
Mtu mwingine aliyenitia hamasa kuendeleza libeneka baada ya kuanzisha blog ni kaka yangu, rafiki yangu na mpiganaji mwenzangu, Fidelis Tungaraza, aka Mti Mkubwa, aka FIDE. Huyu bwana, ambaye anaishi Helsinki, finland, kwa miaka kibao sasa, alikuwa daima akinicharuta mimi na waandishi wenzangu kuwa hatuwatendei haki wadau wa ughaibuni, kwani habari na taswira za nyumbani walikuwa wanazipata kiduchu mno kiasi kwamba ilikuwa sawa na kusema hakuna.

Baada ya hapo, na kama wanavyosema wahenga wetu, kila kitu ni historia. Niliporejea Tanzania nikaanza kufuata maelekezo ya Fide, kwamba niachane na mikutano, makongamano, warsha na mengineyo, bali niwaletee mambo ya jamii. Na ni yeye Fide aliyenipa majina ya Globu ya Jamii na wadau.
Mwaka mmoja baadaye, yaani mwaka 2006, nikiwa jijini New york, nikapata barua pepe toka kwa muasisi wa Globu ya Jamii, kaka Ndesanjo Macha. Akanipa pongezi na pole kwa kuendelea kuteseka na ugonjwa wa Ku-blogu. Pia akanikumubusha kwamba comment moderation nisiache hata siku moja, kwani SERA ya blog inaimarisha blog husika kwa kuzingatia hayo.
Mambo kadhaa yalijiri kuitambulisha Michuzi Blog kwa jamii baada ya hapo. Na mambo hayo yote yaliibuka chini ya kichwa cha habari cha BREKING NYUUUUZZZZZZ……ambapo kila mara hii ilimaanisha kwamba habari na taswira hizi ni za kipekee, za sasa hivi na hakuna ambaye anazo zaidi yangu mimi.
Nachelea kutaja BREKING NYUUUZZZ ZZ zote kwa uhaba wa nafasi, lakini zile za kuuwawa kwa wapendwa wetu Marekani (Nkya na Mazula), Kifo cha Mh Amina Chifupa na kujiuzuru kwa Waziri mkuu Mh Lowassa pamoja na kutajwa kwa baraza jipya la mawaziri ni baadhi tu ya habari moto ambazo Globu ya Jamii iliweza kuwa ya kwanza kutangazia ulimwengu kabla ya mtu yeyote ama chombo kingine cha habari.

Kama nilivyosema awali, mengine yote ni historia. Itoshe tu kusema kwamba nitachukua muda mrefu kueleza kila kitu na nisiweze kueleza robo ya mambo yote. Kwa maelezo hayo naomba ruksa niishie hapa na kuwaomba wadau mbofye sehemu ya ‘KUMBUKUMBU’ na kurejea katika posti za nyuma na kuapata hisoria kamili ya Michuzi Blog. Kila kitu kipo hapo.
Mwisho naomba nisema kwamba Michuzi Blog aka Globu ya Jamii ni mtumishi wa wadau wote duniani. Haichagui wala haibagui, kwani atayetuzika hatumjui. Hivyo nawakaribisha wadau wote tusherehekee siku hii huku nikiwaambia kwamba wakati wa kutimiza miaka 10 (InshaAllah) kutakuwa na MichuziTV na MichuziRadio Online, ambazo ziko njiani hivi karibuni.

Natoa shukrani kwa mdau aliyetoa wazo la kubadili jina ili Libeneke liwe la kimataifa, huku nikimhakikishia kwamba kuwa kimataifa sio lazima lugha iwe tofauti na Kiswahili, kwani tayari watu takriban milioni 400 wanazungumza lugha yetu ya Taifa ambao ndio walengwa wakuu.
Ahsanteni sana wadau kwa sapoti yenu katika muda wote huu na InshaAllah Mola akipenda na panapo majaaliwa MichuziTV na MichuziRadio Online itaibuka hivi karibuni humu humu ndani ya Globu ya Jamii kukuletea mambo kwa sauti na taswira zinazotembea. Tuombeane uzima tu.
Ni vigumu kumshukuru kila mtu aliyechangia mafanikio madogo haya ya Globu ya Jamii. Ila kwa uchache niwashukuru washauri, wachangiaji, walezi pamoja na timu nzima ya Michuzi Blog kwa kufanikisha haya yote.
Nianzie kwa washauri wakuu ambao baadhi ni kama JK, kaka Jeff Msangi wa Bongo Celebrity, Profesa Mark Mwandosya na mama Lucy Mwandosya, Jacob Mwambegele, Freddy Macha, Da'Chemi Chemponda, Balozi Juma Mwapachu, Balozi Peter Kallaghe, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar, Da' Maura Mwingira, kaka Charles Hilary, kaka Abubakar Liongo, kaka Abou Faraji, kaka Ayoub Mzee, Da' Flora Nducha, kaka Freddy Maro, Dr Emmanuel Nchimbi, kaka Hilary Bujiku, Mh Zitto Kabwe, Mh. January Makamba, Mh John Mnyika, kaka Max Melo, Dr Prosper Mosha, Dr Blandina Kilama, Bi Ainde Ndanshau, Da' Teddy Mapunda, kaka Baraka Msiilwa, kaka Frank Eyembe, Da' Sporah Njau, Da' Subi, Da' Jestina George, Da' Mishi Marshall, Kaka Imani Kajura, Da' June Warioba, kaka Assah Mwambene, kaka James Shang'a, Dr Ramadhani Dau, Dr Kashilila, Da' Suzan Mzee, Da'Mariam Mungula, kaka Beda Msimbe, Dr John Shoo, Sensei Rumaza na Sensei Malekia, kaka John Mashaka, Profesa John Mbele, Dr Hassan Mshinda, Da' Mindi Kasiga, Ras Makunja 'FFU', Da'Janeth Mtonyi, Mh Mohamed Dewji, kaka Azim Dewji, Da' Mwamvita Makamba, Da' Taggie Daisy Mwakawago, Kaka David Minja, kaka Ephraim Mafuru, kaka Wilna, Dr Faustine Ndugulile na wengineo kadhaa ambao ni wengi mno.
Kwa kipekee naomba nimshukuru Katibu Mtendaji wa ICGLR Balozi Liberata Mulamula pamoja na kaka Omar Mjenga ambao ndio waliokuwa waratibu wakuu wa Mkutano wa Helsinki Process ambapo Rais wa Tanzania na wa Finland walikuwa Wenyeviti wenza. Asante sana kwa Balozi Mulamula ambaye mpaka leo anaendelea kutoa ushauri kwa Michuzi Blog, pamoja na kaka Mjengwa ambaye japo yuko mbali lakini pia yu karibui nasi daima.
Pia niwashukuru wana Globu ya Jamii wakuu kina Christopher Makwaia 'MK', Francis Dande, Audax Mutiganzi, Woinde Shizza, Muhidin Amri, Othman na Ahmad Michuzi, John Nditi, Prosper Minja, David Owen, Dixon Busagaga, John Mashaka, Dr Hildebrad Shayo, Frank Kallaghe, Othman Mapara, Richard Mwaikenda, Fide Tungaraza, Maggid Mjengwa, Haki Ngowi, Gadna G Habash, Lady JD, Shamim Mwasha, Shear Illusions, Imelda Mwamanga, David Kyungu.
Nawashukuru sana sana sana kwa sapoti yenu. Mie sina cha kuwapa Ila Mola ndiye atayewazawadia kwa wema na ushirikiano wenu.

-MICHUZI
Ankal akipongezwa na Ndesanjo Macha mara baada ya kufungua Michuzi Blog katika ukumbi wa Finlandia hall jijini Helsinki, Sweden, Septemba 8, 2005.
Hongera sana Blog ya Jamii na siku ya kuzaliwa. Na mimi nakubali ushauri aliokupa Macha wa wadau wengine kutaka kutumia blog yako kuumiza hisia wza wengine ni jamba jema sana. Ila umesahahu mara mbili imetokea blog ya jamii ilitumiwa vibaya na wadau bila wewe kujau na ukarekebisha haraka..nakukumbusha.
ReplyDeleteKuna mtu alituma picha ya Dad mmoja London kuwa anatafuta mchumba, kumbe ilikuwa kanyabwoya.
Na nyingine ilikuwa nadhani mwaka huu kwa mdau wa Los Angeles, jina Mushi, kuwa anafanya bishara fulani, naye alikuja kukanusha kuwa haajandika barua pepe, ila ni wadau wabaya kutaka kumchafulia jina. Kwa maneno mengine, mambo hayo yanatokea hata katika magazeti makubwa, kuwa unapewa habari ya kizushi unaitangaza kumbe ni uzushi ( Kumnu Dr Kelly na mwandishi wa BBC) nk. Kwa hiyo funga mkanda, dhibiti maonai ya wadau, kwani wengine nia sio nzuri kwa wenzao au blogu ya jamii.
Kity cha mwisho nakupongeza, ni kuwa wewe kuchagua lugha yako, na bila kuyumba hata pale wadau wengine walijaribu kutukana au kusaga na ukachapisha mawazo yako. wewe kusema 'kijifakesheni' sio kwamba hujui kiswahili fasaha, ila waleo waliokosoa ndio hawajui..binafsi lugha ya Blog jamii inaleta mwamko na hamu ya kuisoma, na hasa kuzingatia heshima ya wadau unayoshikilia .
Mungu ibarikia Blog ya jamii an wenzi wake
Anko Helsinki iko Sweden?
ReplyDeleteNatuma mara ya pili hongera kwa Michuzi ya kwanza imekataa hapahapa lakini kabla ya kuendelea nakuchapa kitaaluma katika 'caption' imeandikwa kwa makosa Helsinki -Sweden badala ya Finlandia! Baada ya sahihisho ND SPIKA NAPENDA KUTOA HOJA KUMPONGEZA MSHIKAJI HUYU MBUNIFU MWENYE ASILI YA KERLI KAMA MIMI KWA KUTUTOA TONGOTONGO ILE MBAYA! Napenda kuchukua fursa hii kutoka ombi la kadamnasi kuwa mimi pia ninayo 'ka-blog' kangu kanaitwa MKATAMITI je ni fanyeje nayo ikue ifikie japo moja chini ya nane ikilinganishwa na MICHUZI BLOG! NAREJEA KUSEMA MSHIKAJI MWANARELI HONGERA SANA NA UKOLEZE ZAIDI MOTO WA KOLEO...USIVUNJIKE MOYO ABADAN ENDELEZA LIBENEKE KAMA KAZI..! HONGERA MSHIKAJI..! TEHEEHEEE..!
ReplyDeleteMidlajy Maez a.k. MKATAMITI - ulitsakholzunova@gmail.com
Anko nadhani ulimaanisha jiji la Helsinki Finland na sio Sweden.
ReplyDeletePongezi ankal kwa kazi nzuri unayoifanya. Tunakuomba uendelee hivyo hivyo na tunamwomba Muumba wetu wote akuzidishie uwezo wa kuendelea kufanya kazi yako nzuri. Kila la heri.
ReplyDeleteNapenda kuchukua nafasi hii kuipongeza Michuzi Blog kwa kufikisha miaka sita. Happy Birthday!
ReplyDeleteKaka, BIG-UP katika siku ya kuzaliwa blog yako. wengine tunakiri kupata ufahamu na changamoto kutoka kwako. Kama ulivyotufahamisha kwamba ulipata kutoka kwa Macha na Fide... Hongera sana, pia nakupongeza kwa kututoa tongotongo... Ila pia ningependa kukukumbusha vitu vitatu katika maisha yetu hapa duniani, navyo ni:-
ReplyDelete1. Ukiwa huna mshiko hakuna shida, ila unapokosa fikra sahihi hapo "u a in trouble".
2. hakuna swali la kijinga, ila kuna jibu la kijinga na bovu siku zote. Ni wajibu wako kuwaelimisha wadau na si kuwaponda!
3. Tunachohitaji katika kufanikisha maisha yetu ni kutumia akili zetu vizuri na kwa wakati.
Kaka kila la kheri... tupo pamoja!
Toka tarehe 8/9/2005 mpaka 8/9/2011 ni Miaka sita sasa! Big up Michuzi!
ReplyDeletehttp://issamichuzi.blogspot.com/2005/09/michuzi-and-ndesanjo.html
Hongera sana Kaka Michuzi....MICHUZI BLOG OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE......MICHUZI BLOG OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE....MICHUZI BLOG OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!...mdau Canada
ReplyDeleteHappy Birthday Michuzi Blog, huu ni kama moto wa nyika ulianza taratibu, wapo wengi walio beza hizi blog wakidhani ni ucharii tu lakini hawakuwa wanasoma alama za nyakati katika nyanja ya mawasiliano katika karne hii ya sayansi na teknolojia, walipuuza wakati ule lakini ndio hao sasa wanakimbizana kufungua blog zao.
ReplyDeleteHivi sasa kila mwenye wavuti ana blog pia, Kuanzia White House ya Washington mpaka kwetu Magogoni, wapo wenzetu wengi ambao wamekuwa wanaendesha maisha kupitia ku-blogs, hii ndio hasa maana ya Zama za Mawasiliano, blog zimekuwa kiungo kikubwa mmno katika upashanaji wa habari duniani, waweza kurusha habari popote pale ulipo kuelekea ulimwenguni, haijalishi wapi unaishi, kijijini au katikati ya jiji, bado waweza kuwasiliana na ulimwengu.
Wengine tuliona hii kitu tukaamua kukujaribu takaingia mzigoni kwa kutiwa hamasa nawe Ankal Michuzi, muda si mrefu Bongo Pix Blog nayo itakuwa inatimiza miaka sita pia, hongera kwa kutimiza miaka hii sita lakini zaidi hongera kwa kuleta na kuhamasisha upepo huu wa mabadiliko katika tasnia nzima ya habari na upashanaji habari.
Long Live Michuzi Blog.
uzuri wako Ankal michuzi ni mmoja....UNAJUA KUSHUKURU....mwenyezi mungu akuzidishie hekima na busara pia akupe maarifa yakuendeleza blog yetu pendwa ya jamii katika viwango vya kimataifa...
ReplyDeletechonde kamwe usilewe umaarufu....maana itapelekea mauti ya blogu yetu tukufu....
mwisho kabisa,kaka michu fanya hima jamani kuanzisha hiyo michuziTV na Radio maana nahisi redio na TV station zote za bongo zinaitaji kuamshwa....hii itakupa nguvu "kimshiko" ili uje na libeneke kamili "kampuni ijitegemeayo ya habari"
May God bless Michuzi Blog....
by tha way,kaka michu ukuu wa wilaya wa nanii hiii umeshakwisha au wamekuchakatua...heheheeh lol
ni mimi,
Waitara Chacha
Vietnam