Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wanne wanao ziwakilisha nchi hapa Tanzania.Walioziwasilisha hati zao leo ni pamoja na Balozi Luiz Javier Campuzano wa Mexico, Balozi Geoffrey Peter Tooth wa Australia,Balozi Sinnika Antila wa Finland na balozi Hossam Eldin Moharam wa Misri.Pichani balozi Bi. Sinikka Antila wa Finland akiwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo katika makazi ya balozi wa Cuba nchini Tanzania,Oysterbay jijini Dar es Salaam, kufuatia kifo cha Makamu wa Rais wa Cuba,Jenerali Julio Casa Regueiro.Aliyesimama Pembeni ya Rais ni Balozi wa Cuba nchini Tanzania Mhe.Ernesto Gomez Diaz(picha na Freddy Maro)

kumbe adi ubalozi wa mexico upo bongo , hivi kwani kuna raia wengi wa mexico au cuba bongo , mtazamo wangu ni zinani kama kuna hao raia sana bongo. so ubalozi wa kama mexico una kazi gani bongo , kwani mimi najua sababu moja kubwa ya ubalozi kuwepo sehemu ni wengi wa raia wa nchi hiyo kuwepo kwa mfano wachina wapo bongo wengi pia wanafanya business trade sana na tanzania. je kuna huusiano gani kati ya mexico na tanzania?
ReplyDeletemsaada kwenye tuta jamani kuusu hili jambo.
mdau china
Poleni, rafiki wa kweli.
ReplyDelete