Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Bw. George Masaju akifungua semina ya Wahariri wa Vyombo vya habari nchini iliyolenga kuwafahamisha kuhusu kusaidia kuandika habari juu ya haki za binadamu. Semina hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Masuala ya mahusiano ya Katiba na Haki za Binadamu kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Mathew Mwamu.
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alberic Kacou akisoma hotuba katika ufunguzi wa Semina ya Siku ya Wahariri wakuu wa vyombo vya habari nchini ambapo alisisitiza ushirikiano katika nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa Tanzania ikiwa ni nchi moja wapo kusimamia, kusaidia na kuhamasisha utetezi wa haki za Binadamu chini ya Mpango wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa Semina hiyo imefanyika kwa ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa nchini na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Kulia ni Mkurugenzi wa Masuala ya mahusiano ya Katiba na Haki za Binadamu kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Mathew Mwamu.
miongoni mwa Wahariri Wakuu wa Vyombo mbalimbali vya habari nchini wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na watoa mada katika Hoteli ya Double Tree By Hilton jijini Dar es Salaam.
Jopo la Wahariri Wakuu wa Vyombo vya habari wakiwa katika semina elekezi juu ya haki za Binadamu iliyoratibiwa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Umoja wa Mataifa nchini.
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alberic Kacou akibadilishana mawazo na Mhariri wa Makala wa Gazeti la Serikali la kila siku (Daily News) Deogratius Mushi.
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alberic Kacou akifanya mahojiano na kituo cha Televisheni cha TBC1.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. TBC1 should modenize, hii mzinga wa Cam unamwumiza bwana paparazi

    ReplyDelete
  2. Ako naomba jamani mtupe updates za ndugu yetu Hasheem Thabeet anaendeleaje uko NBA , naona sikuizi kimiya sana , bado na ndoto japo hata kuona clip ya huyu ndugu yetu akicheza NBA kwani sijawahi kuona , hila nasikia tu kuna mtanzania NBA.
    thanks
    mdau Singapore

    ReplyDelete
  3. YANI WATANZANIA BWANA HATUPO SERIOUS KABISA,ORGANIZATION KUBWA KAMA HII WAMESHINDWA KABISA KUFIKIRIA KUWA WAZUNGUMZAJI WATAHITAJI KISIMAMIZI CHA MICROPHONE?MAMBO YA MIAKA YA 70 YA MTU KUSHIKIWA MIC,PLEASE JAMANI VITU VIDOGO KAMA HIVI VINATUFANYA WAGENI WANASHINDWA KUTUELEWA HOW ORGANIZED WE ARE,NACHOKA NA VITU VYA AJABU AJABU KAMA HIVI

    ReplyDelete
  4. MIC BADO ZINATUMIKA HATA UGHAIBUNI HUSUSAZ NJE YA STUDIO. CAMERA NDIO WANAWEZA KUNUNULIWA MPYA, LAKINI PESA ZIKO WAPI? TBC WENYEWE HAWAWEZI KUJIENDESHA WANATEGEMEA KODI!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...