Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania waishio New York,New Jersey,Connecticut na Pennsylvania Ndugu Hajji Khamis na Uongozi wake wakishirikiana na Ubalozi wa Tanzania umoja wa mataifa walifanya ibada ya kuwaombea waathirika wa ajali ya meli iliyotokea Zanzibar jumamosi ya tarehe 10 septemba na kuuwa abiria wasiopungua 250.
Ibada hiyo iliwakutanisha watanzania wa dini za kikristo na kiislam wakiongozwa na mkuu wa wachungaji wa eneo la Mount Vernon,New York Mchungaji Mama Carol Fryer kwa upande wa wakristo na Ustadh Masoud Maftah kwa upande wa waislam.
Akielezea kuguswa kwake na tukio hilo Mchungaji Carol Fryer aliifananisha ajali hii na tukio la september 11,2001 kwa Marekani,vilevile aliwasisitiza Watanzania wasiache kuwaombea dua waathirika wa ajali hii.Mchungaji Carol Fryer aliwahi kuishi Tanzania hivyo alisisitiza Watanzania waendeleze upendo baina yao.
Akitoa nasaha zake Ustadh Maftah aliwasisitiza Watanzania kuungana wanapokutwa na msiba kama huu wa kitaifa bila kujali imani zao.Alimalizia kwa kuwasalia(salatul ghaib) waliopoteza maisha katika ajali hiyo.
Ibada hii vilevile ilihudhuriwa na Ndugu Seruhere aliemwakilisha Mh.Balozi Ombeni Sefue mwakilishi wetu umoja wa mataifa.Balozi Sefue alieleza masikitiko yake kwa kutoweza kuhudhuria kutokana na kutingwa na kazi nyingi lakini alisisitiza mshikamano na upendo kwa Watanzania.
Pia alikuwepo muwakilishi wa Muheshimiwa Asha Rose Migiro,Naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa,Balozi Manongi kwa niaba yake pamoja na kueleza kuguswa kwake na ajali hiyo,alihimiza mshikamano kwa Watanzania.
Wengine waliohudhuria ni bwana Richard Kasesela aliyekuja kushiriki katika mkutano wa Umoja wa mataifa nae alielezea kwa ukaribu zaidi msiba huu kwa kuwa ulipotokea alikuwa nyumbani Tanzania na vilevile Bwana William Malecela na Dr.Abas Byabusha walipata nafasi ya kuzungumza machache juu ya msiba huo.
Katika kufunga ibada hiyo Mwenyekiti Ndugu Hajji Khamis alimalizia kwa kuwashukuru wale wote waliopata nafasi ya kuhudhuria ibada hiyo na akizindua accounti maalum kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa ajali hiyo ambayo itasimamiwa na jumuiya yake,aliwaomba Watanzania kila kona wajitokeze kuwachangia waathirika ili na wao wapate kufarijika kwa kuwa msiba huu ni wa kitaifa na unamhusu kila mwenye utanzania.
Taarifa kamili za accounti hii maalum zitawekwa kwenye blog za Michuzi na Vijimambo ili iwe rahisi kwa watanzania wote kuchangia popote walipo.
Account ilianza kwa michango ya Dola mia saba zilizochangwa hapohapo. Akielezea zaidi alisema ibada hiyo ni ya kuwaombea wale waliotangulia na majeruhi na pia kuwafariji wale waliopotelewa na jamaa zao wa karibu zaidi.
Nawapongeza wenzetu walioughaibuni kushiriki ktk misaada ya majanga lakini napenda watupatie misaada ya elimu ya kuzuia majanga. Michango ya kifedha inaweza kutumika hata vibaya lkn elimu na mwamko utatufaa zaidi. Waswahili tumekuwa walizi mno kuliko kuwa waepukaji wa majanga.
ReplyDeleteNa makampuni ya bima yahusike ktk fidia kwani ndio wajibu wao.