MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Kamanda wa Vijana wa CCM Kata ya Kivukoni Dar es Salaam, Sharik Choughule baada ya kamanda huyo kukabidhi mchango wake wa sh. milioni moja, kuchangia Mfuko wa Watu Walioathirika kutokana na ajali ya kuzama kwa meli ya M.v Spice Islander, iliyozama Nungwi, Unguja, wiki iliyopita ikiwa safarini kwenda Pemba.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akipokea mchango wa sh. milioni moja kutoka kwa Kamanda wa Vijana wa CCM Kata ya Kivukoni, Dar es Salaam, Sharik Choughule, ikiwa ni mchango wake kwa Mfuko wa Maafa kwa Watu Walioathirika kutokana na ajali ya kuzama kwa meli ya M.v Spice Islander, iliyotokea Nungwi, Unguja wiki iliyopita. Alikabidhi mchango huo, jana.
KAMANDA wa Vijana wa CCM kata ya Kivukoni, Dar es Salaam, Sharik Choughule akimjulia hali mmoja wa majeruhi walionusurika katika ajali ya meli ya M.v Spice Islander, Abdalla Juma Sadik, ambaye amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Zanzibar. Choughule alikwenda Zanzibar kuchangia Mfuko wa Maafa kwa Waathirika wa ajali hiyo, iliyotokea wiki iliyopita, Nungwi, Unguja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...