Kijana David Richard akitambulishwa na mshereheshaji Rosemary Mwakitwange wakati akitambulisha libeneke lake la G Networking Company linaloendesha mygloblink.com katika kiota cha maraha cha Mafian Fish lounge kilichopo Masaki, jijini Dar es salaam. Globu ya Jamii inampongeza David kwa ushupavu wake wa kudiriki kuja na libeneke ambalo kwa jinsi alivyolipangilia, kijana huyu atafika mbali sana sana. Nasi tunamuahidi ushirikiano wa karibu katika safari yake hiyo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Twamkaribisha sana kwenye uwanja huu wa mapambano

    ReplyDelete
  2. Amekoses kigodo. Kaandika "We here to entertain you" badala ya "We are here to entertain you"

    ReplyDelete
  3. Kama mmoja wa social networkers, nampa hongera sana and wish him all the best. Welcome to the world of social media. Ila ingekuwa vizuri kama angeweka "contents" za kutosha kwanza kabla ya kuzindua hiyo site to the public. Kwa sasa mtu akiitembelea hakuna mengi sana ya kusoma au kuangalia. Ni kama vile ipo empty. Kabla ya kuzindua ingebidi labda kuwe na "contents" kidogo so visitors can browse around. Kwa mfano ukiangalia kwenye forums kuna thread tatu tuu. It can take more than a year to have a site rich in content.

    Pia wakati anaizundua hii site ilibidi watu wawe wanajiunga hapo hapo kwenye kiota. Badala yake kwenye picha nimeona kama watu wakikata kinywaji kwa kwenda mbele. Labda ni kwa sababu ya eneo na muda aliochagua kuzindua hiyo site? Ajaribu kuangalia ile filamu ya The Social Network labda anaweza kupata hints jinsi Facebook walivyofungua na kupanua mtandao wao.

    Mwisho inabidi aanze kuweka mikakati mapema kabisa. Does he want to run the site for fun or for profit? This is very important asije akawa disappointed baadae. Others, we like doing it for fun. Mengine ni matokeo. Michuzi, moja ya maveterani wa social media, anaweza kukupa hints though sijui kama ana charge. LOL.

    ReplyDelete
  4. Thank you alot for your comments guys. And thank you for welcoming me. About the content. More its coming and me and my team will be working hard to provide you the best of the service to satisfy your needs.

    Cheers..

    Thank you alot. Thank you brother Michuzi. Thank you all my funs.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...