MHESHIMIWA BALOZI WA AFRIKA YA KUSINI, DR. ZOLA SKWEYIYA AKIWEKA SAINI KWENYE KITABU CHA MAOMBOLEZO
MHESHIMIWA BALOZI WA TANZANIA, BWANA PETER KALLAGHE ALIBADILISHANA MAWAZO NA MHESHIMIWA BALOZI WA AFRIKA YA KUSINI,DR. ZOLA SKWEYIYA.
KITABU CHA MAOMBOLEZO KWA WAHANGA WA MELI YA SPICE ISLAND KIMEFUNGULIWA RASMI JANA KATIKA OFISI ZA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA.
MABALOZI WA NCHI MBALIMBALI NA MARAFIKI WA TANZANIA WAMEUNGANA NA NDUGU ZAO WA TANZANIA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MSIBA, WAMEANZA KUFIKA OFISINI HAPO KUWEKA SAINI KWENYE KITABU CHA MAOMBOLEZO.
BAADHI YA WALIOFIKA JANA KWENYE OFISI HIZO, ALIKUWA MHESHIMIWA BALOZI WA AFRIKA YA KUSINI HAPA NCHINI UINGEREZA, DR. ZOLA SKWEYIYA, NA BALOZI WA GAMBIA.
WATANZANIA WOTE NA MARAFIKI WA TANZANIA MNAOMBWA KUFIKA OFISINI HAPO KUWEZA KUWEKA SAINI KWENYE KITABU HICHO CHA MAOMBOLEZO AMBACHO KITAKUWA WAZI MPAKA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 17/09/2011. MUDA NI KUANZIA SAA 10.00am – 16:00pm.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...