Mzee Shauri Timoth Nathan (18/08/1925 - 18/09/2007)
Mroki Mroki
Sekunde, Dakika, Saa, Siku, Wiki, Mwezi, Mwaka na hatimaye mika minne sasa imetimia tangu Mzee Shauri Timoth Nathan (18/08/1925 - 18/09/2007) ututangulie Mbele za haki kama ulivyotutangulia kuja duniani Tarehe 18/09/2007 saa kumi na mbili jioni.

Nimajonzi sana kwetu hasa ukizingatia kuwa uliondoka katika tarehe ambayo kitinda mimba wako Mroki Mroki alizaliwa na ni siku kumi tu baada ya kufunga ndoa Mroki.
Unakumbukwa na wengi sana maana ulikuwa ni mhimili mkuu katika familia, kipekee ni Mke wako Mary O Nathan na watoto wako James Nathan, Mrs Stella Kaluse, Lloyd Atenaka, Dossa Mroki,Freddrick (Kajiru) Mroki, Onesmo Nathan, Thomas Nathan, Daniel Nathan, Kyaze Nathan, Namche Mroki, Kille Nathan na Mroki Mroki na Wakwe zako wote.
Pia unakumbukwa sana na Wajukuu zako Kidai Kaluse, Shauri Kaluse, Mfaume Kilangi, Shauri James, Mwanaamani James, Hellena James, Nuru James, Maria Kaluse, Ludao Kaluse, Kilave Atenaka, Maria Atenaka, Victoria Dossa, Doureen Atenaka, Erick Mushi, Beatrice Mroki, Timothy Tomas, Timothy Kajiru, Timothy Kille, Maria Thomas Irine Atenaka, Anjela Chistian, Glory Mroki, Nathan Kyaze, Nathan Dossa, Dinner Onesmo, Debora Daniel na Leonard Kyase pamoja na Vitukuu wako pia kutoka kwa Mwanaamani na Shauri.

Tunakumbuka maneno yako ya Mwisho uliotuachia watoto wako kuwa TUPENDANE, TUSAIDIANE na TUSHIRIKIANE, baba hakika hili linatendeka na tupo na umoja uliotujengea na tunajivunia hilo.
Tunazidi kukuombea Baraka na pumziko jema maana sote uliotuacha tutakufata kama tulivyo kufuata hapa duniani.
Jina la Bwana Lihimidiwe Amina.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nilishtuka nikadhani na huyo wa chini nae kafariki.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...