Mabalozi wanaowakilisha nchi zao kutoka nchi mbali mbali duniani kutoka Afrika,Ulaya,Asia,Marekani ya Kusini na Kaskazini na nchi za Ghuba hapa Marekani,wamefika katika Ubalozi wa Tanzania(TANZANIA HOUSE) uliopo Washington,DC kujumuika katika kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia msiba mkubwa ulilikumba Taifa la Tanzania kufuatia kuzama kwa meli ya MV Spice Islander katika mkondo wa Nungwi ,Zanzibar. Mabalozi hao kwa wingi wakiongozwa na mabalozi kutoka Zimbabwe,Bahrain,Nicaragua,Namibia,Spain,Swaziland,Fiji, Spain,Mexico,Oman, Russia na kadhalika walionyesha kuguswa na ajali hiyo na kwa pamoja waliwaombea wahanga wa ajali hiyo na kuwaomba wafiwa pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa na subira katika wakati huu huu mgumu kutokana na ajali hiyo mbaya katika historia ya usafiri wa majini visiwani Zanzibar.
Home
Unlabelled
MABALOZI WATIA SAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO,UBALOZI WA TANZANIA,WASHINGTON,DC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
raia wa kawaida wa kitanzania wataruhusiwa lini ku sign hicho kitabu hebu tujulisheni jamani.mtanzania aishiye new york
ReplyDelete