Mkuu wa shule ya sekondari Shauritanga Mwl. Kalist Shirima akiwaonesha wanahabari (hawapo pichani)eneo ambalo lilikuwepo bweni la wanafunzi la mwanzo katika shule hiyo lililoungua moto.
 Kaburi la pamoja walilozikwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Shauritanga baada ya kuungua moto wakiwa bwenini.
 Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Shauritanga wakiimba wimbo wa shule
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Balozi Athuman Mhina(mwenye taji lenye rangi nyekundu)aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya shule hiyo akiwa na mwenyekiti wa jumuiya ya
wazazi mkoa wa Kilimanjaro Bw. Thomas Ngawaiya.
Wanafunzi katika mahafali hayo.

Na Dickson Busagaga wa Globu ya Jamii
MAHAFALI ya 32 ya wahitimu 77 wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Shauritanga, yalitanguliwa na sala maalumu ya  kuwakumbuka wanafunzi zaidi ya 40 waliofariki dunia kwa ajali ya moto Juni 18, 1994.

Aidha wazazi na wanafunzi waliohudhuria mahafali hayo mwishoni mwa wiki, walipata fursa ya kutembelea kabuli la pamoja walilozikwa wanafunzi hao ikiwamo kupiga picha za ukumbusho huku baadhi yao
wakibubujikwa na machozi baada ya kuliona kaburi hilo.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao ndiyo wamiliki wa shule hiyo, Balozi Athuman Mhina, ndiye aliyeongoza sala hiyo maalumu pamoja na kumkumbuka mwanzilishi wa shule hiyo,
Padri Aloyce Shauritanga.

Akizungumza katika mahafali hayo, Balozi Mhina alisema shule za jumuiya hiyo zilianzishwa mahususi kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi waliokosa nafasi za kujiunga na elimu ya sekondari katika shule za
serikali.

Alisema kuanzishwa kwa shule hizo kulikuwa na changamoto nyingi ikiwamo kubezwa na baadhi ya watu kwamba jumuiya hiyo inachukua ‘makapi‘ wakimaanisha wanafunzi walioachwa kuchaguliwa kujiunga na
shule za sekondari za serikali.

Hata hivyo, alisema pamoja na kubezwa huko, hivi sasa shule nyingi zinazoendeshwa na jumuiya hiyo zimekuwa na mafanikio makubwa kielimu na tangu kuanzishwa kwake mwaka 1977, zaidi ya wanafunzi 3,500
wamejiunga na vyuo mbalimbali nchini.

Awali, mkuu wa shule hiyo, Kalist Shirima, alisema pamoja na mafanikio hayo bado kuna changamoto zinazoikabili shule hiyo zikiwamo uhaba wa vifaa vya  kufundishia na kujifunzia hasa vitabu, upungufu wa nyumba
za walimu na uhitaji wa mabweni ya kisasa kwa ajili ya wanafunzi wa
kike.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...