WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS MAHUSIANO NA URATIBU WA SERIKALI YA MUUNGANO MHE, STEVEN WASSIRA KWA NIABA YA FAMILIA YAKE AKIKABIDHI MCHANGO WAO WA SH, MILIONI MBILI KWA MWENYEKITI WA KAMATI YA MAAFA KITAIFA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI KUSAIDIA MFUKO WA MAAFA KUFUATIA KUZAMA KWA MELI YA MV. SPICE HIVI KARIBUNI.

Na Mwandishi Wetu,Zanzibar.


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuwa makini katika kuhakikisha Maisha ya Wananchi wanaotumia usafiri kwa Njia ya Bahari unakuwa salama na wakuaminika.

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wana habari kufuatia tatizo la hitilafu ya kiufundi lililoikumba Meli ya M.V Serengeti iliyokuwa ikijiandaa kusafirisha Abiria kuelekea kisiwani Pemba jana usiku.

Balozi Seif Ali Iddi alilazimika kutoa agizo la kuzuiwa kutosafiri kwa meli hiyo baada ya kupata taarifa za hitilafu kwenye chombo hicho hadi hapo kitakapofanyiwa marekebisho.

“ Nimemuamuru Katibu wangu aende Bandarini Kuwasiliana na Wahusika wa Meli hiyo ili chombo hicho kwanza kifanyiwe marekebisho kutokana na tatizo lililojitokeza na baadae ndio kiendelee na safari zake ” Alisema Balozi Seif Ali Iddi .

Makamu wa pili wa Rais Amekemea tabia ya baadhi ya wafanyakazi wa vyombo vya usafiri wa Baharini ya kushutumiwa kuwazuia Wasafiri kuteremka kwenye chombo wakati yanapojitokeza matatizo kwenye chombo wanachosafiria

Balozi Seif Amesema Abiria ana haki na maamuzi ya kuteremka kwenye chombo wakati wowote mradi akishaona kwamba usalama wake uko mashakani.

Amezikumbusha mamlaka zinazoshughulikia usafiri wa njia ya Maji kuhakikisha zinafanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuona vyombo wanavyovisimamia vinafanya shughuli zake kwa njia ya usalama.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameendelea kupokea michango kutoka kwa wahisani mbali mbali kusaidia Kamati ya maafa kufuatia ajali ya Meli ya M.V Spice iliyotokea hivi karibuni.

Waliotoa michango hiyo ni pamoja na Bodi yaWadhamini wa Mfuko wa Pencheni kwa Watumishi wa Umma Tanzania { PSPF }, jumuiya ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Uongozi wa Kampuni inayosimamia Hoteli tatu za Kitalii za Breeses,Baraza, Palm na Rich son Diving Centre, pamoja na Uongozi wa Kamati ya Mamendeleo ya Kijiji cha kiwengwa.

Wengine waliochangia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu wa Serikali ya mauungano yeye na familia yake Mhe, Steven Wassira. pamoja na Idara Maalum inayosimamia Vikosi vya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Wawakilishi wa Taasisi hizo wameelezea kuguswa kwao na msiba huo ambao ni wa Wananchi wote.

Akitoa shukrani zake Mwenyekiti wa kamati ya Maafa Zanzibar Balozi seif amesema mchango huo utafanyiwa kazi kwa nia thabiti iliyokusudiwa.

Balozi Seif ametoa pongezi maalum kwa vikosi vya ulinzi hasa vile vya SMZ kwa namna nzima ya ushiriki wao katika uokozi wa wananchi walipatwa na maafa hayo.

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi amekutana na Balozi wa Israel Nchini Tanzania Bwana Kasbian Nuriel Chirich.

Katika mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Israel na Zanzibar kwa jumla.

Balozi Kasbian amemueleza Balozi Seif kwamba Zanzibar bado ina nafasi kubwa na ya pekee ya kujitangaza kwa Israel hasa katika masuala ya Uwekezaji katika eneo la Utalii na Bahari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Serikali ya zanzibar haikupata fundisho lolote katika maafa yaliyotokea wiki chache zilizopita?

    Mbali ya kuwa meli ilikuwa imejaza abiria, uokozi wa abiria ulichelwa mno kwa sababu ajali ilitokea usiku na jeshi la uokovu na wananchi waliojitolea hawakuweza kuwafikia abiria kwa sababu ya ukosefu wa vifaa ikiwa pamoja na vifaa vya mawasiliano na vifaa vya mwangaza.

    Wananchi wangelitegema hadi pale serikali itakapoweza kutatua matatizo haya usafiri wa baharini visiwani utakuwa ni wa saa za asubuhi hadi jioni na sio usiku. Kama serikali ya zanzibar hawajalifikiria hili kuna haja ya serikali ya tanzania kuingilia kati mara moja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...