Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, wakati walipokutana katika viwanja vya Maisala, walipofika kutembelea mabanda ya kupokelea miili ya watu waliofariki katika ajali ya meli ya Spice jana Septemba 10.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wakazi viongozi na wakazi wa Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakati alipofika katika eneo hilo kwa ajili ya kuwafariji wakazi hao waliopatwa na matatizo pamoja na kukagua shughuli za uokoaji, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika Viwanja vya Maisala mjini Unguja, wakati alipotembelea katika eneo hilo lililokuwa likitumika kupokelea miili ya watu waliofariki katika ajali ya meli ya Spice jana Septemba 10.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea na kukagua maeneo yaliyokuwa yakitumika kupokelea na kuhifadhi miili ya watu waliokufa katika ajali ya meli ya Spice, pamoja na majeruhi waliokuwa wakipitishwa katika eneo hilo la Ufukwe wa   Bahari ya Hindi Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Natoa pole kwa wafiwa wote na namuomba Mungu awalaze pema wote waliopoteza maisha yao. Amen. M Chuwa Arusha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...