Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya Tazara kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Maonyesho hayo yamefanyika leo Septemba 14 katika Viwanja vya Tazara jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Uchukuzi miaka ya nyuma, Job Lusimbe, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake katika ujenzi na maendeleo ya Reli ya TAZARA, wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya Tazara kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Maonyesho hayo yamefanyika leo Septemba 14 katika Viwanja vya Tazara jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mzee John Nchimbi na mkewe, Sylviaa Nchimbi, waliokuwa ni abiria wa kwanza kusafiri na Reli ya TAZARA mwaka 1976, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake katika ujenzi na maendeleo ya Reli ya Tazara, wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya Tazara kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Mzee Nchimbi na mkewe wamepewa zawadi ya kusafiri na treni ya TAZARA bure katika kipindi chote cha maisha yao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Tazara, Mkandarasi Abdallah Shekimweri, wakati akitembelea mabanda ya maonyesho kwenye maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya Tazara na maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania katika viwanja vya TAZARA jijini Dar es Salaam leo Septemba 14.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoka katika moja ya mfano wa Behewa la Daraja la kwanza la Treni ya TAZARA, wakati alipokuwa katika maonyesho ya TAZARA, wakati wa maadhimisho ya miaka 35 ya shirika hilo sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania, iliyofanyika katika viwanja vya TAZARA jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Tazara, Mkandarasi Abdallah Shekimweri, kuhusu matumizi ya Kibelenge wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho kwenye maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya TAZARA kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Maonyesho hayo yalifanyika leo Septemba 14 katika Viwanja vya Tazara jijini Dar es Salaam.
Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu mataluma ya Reli na matumizi yake wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho kwenye maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya TAZARA, kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Maonyesho hayo yamefanyika leo Septemba 14 katika Viwanja vya Tazara jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Tanzania tuna maneno mengi kuliko vitendo na ndiyo maana hatuendelei. Hapa kinachotakiwa ni kueleza ni jinsi gani au TAZARA ina mikakati gani ili kuifanya ifanye kazi yake ipasavyo, manake sasa shirika linakaribia kufa.

    ReplyDelete
  2. Hahahahaha, kweli nashindwa kuelewa sasa tulipo. Mpaka vibelenge bajaji

    ReplyDelete
  3. Tazara imeoza, sasa kinachosherewa ni mafanikio au nini, miaka 35 na hali halisi ya sasa ni vitu viwili tofauti. Sioni sababu ya kufanya sherehe, kwa mafanikio gani??. Kaeni kimya mfanye mipango ya kuifufua tazara. Maroli yanaaribu barabara sababu treni zetu hazifanyi kazi. Mnamchosha Magufuri bure. Barabara zinatengenezwa hazitakaa muda. Hata ajili za barabarani zimezidi sababu treni hazifanyi kazi sawa sawa kama vipi mrudishieni mchina, kubalini mmeshindwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...