MFUASI wa CCM, Mussa Tesha (24) akiwa katika hospitali ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora, leo. Tesha ameungua usoni na sehemu kadhaa mwilini baada ya kumwagiwa tindikali usiku wa kuamkia leo na watu wanaodaiwa kuwa ni wafausi wa CHADEMA, ambapo inaelezwa kuwa walimwagia tindikali hiyo alipokuwa katika harakati za kubandika mabango ya mgombea wa Ubunge jimbo lgunga kwa tiketi ya CCM katika mitaa ya jimbo hilo. Tesha anatarajiwa kuhamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo kwa gharama za CCM.Anayemtazama ni Daktari wa hospitali hiyo, Selemani Masinga.
Home
Unlabelled
mfuasi wa CCM amwagiwa tindikali IGUNGA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



Natoa pole zangu kwa Ndugu Tesha. Jamani tutumie nafasi zetu kihalali pasipo kuumizana kiasi hiki. Hii ni chuki ambayo haitakwisha kwa vitendo vibaya kama hiki. Mungu aonaye sirini anajua na ameona kilichotendeka. Kweli haifai naman hii. POLE SANA NDUGU YANGU.
ReplyDeleteNAMNA HIYO HALAFU CHADEMA WATAWALE NCHI HUU NI UNYAMA WA HALI YA JUU HIVI VYAMA VYOTE VIPO KISHERIA INAKUWAJE WATU WAANZE KUUWANA KWA KUPEANA VILEMA KWA SUMU YA TINDIKAEI INA MAANA WALIPANGA NA WANAYO NYINGI YA KUFANYIA UNYAMA KAMA HUO WALIOUFANYA NDIO MAANA TUNASEMA CHADEMA HAWAJAKOMAA KISIASA KUANZIA VIONGOZI WAO HADI HAO AKINA KAJAMBA NANI NDUGU WANA IGUNGA DAWA NI KUWANYIMA KULA CHADEMA HAWANA MAANA HATA KIDOGO KILA SIKU WANAOTA KUTAWALA NCHI WANAONA HAWAFANIKIWI WANAZUSHA MAMBO WANAONA HAWAUNGWI MKONO WANAWATIA VILEMA WAPIGA KURA WAHUSIKA JE KUNA MAANA YA KUWACHAGUA CHADEMA? PIGA UWA HAWAFAI HATA KIDOGO KAZI KWENU WANA IGUNGA mdau ughibuni
ReplyDeleteHizi siasa za kutoana kafara sasa tuziache. Wewe unayesema waliomwagia ni wafuasi wa CHADEMA una uhakika gani kama si wafuasi wenzake wa CCM waliokuwa wanagombea tenda ya kubandika mabango?. Tupingane bila kuumizana na njia pekee ni kuhakikisha kuwa haki inatendeka katika kumpata mshindi halali wa uchaguzi. Ujanjaunja wowote ule utaacha makovu miongoni mwetu. Hakuna kusema kuwa huyu CCM, CUF au CHADEMA tuweke mbele utaifa atakayeibuka mshindi ni mtanzania sasa kwa nini tuanze kupofuana na kuharibiana maisha?. Yale mambo ya ushindi lazima au kwa vyovyote tuyaache. Tuwaache wananchi wajichagulie mbunge wamtakaye. Ninajua kuwa CCM hawatakubali kushindwa uchaguzi huu na sababu kubwa ni siasa. Timu mpya iliyoingia madarakani itataka kuonesha kuwa wanafanya kazi. Ila kitu cha kujua hapa ni kwamba wananchi ndiyo waamuzi si viongozi wa chama.
ReplyDeletePole sana Mussa, hata serikali yote ikifika kukupa pole bado macho hayo yapo matatani. Cost yako wanaijua wazazi wako. Kilichoniudhi kwenye post hii ni kuweka conclusion kuwa wahusika ni CHADEMA lengo likiwa kuanza unyanyasaji wa kuwakamata wafuasi wa CHADEMA wasifanye siasa. Hii ni hatari kwa ustawi wa demokrasia yetu. Maswa ilikuwa hivyohivyo mkamuweka ndani Shibuda, sasa mmepeleka Nzega tactic hizi. Shame on everyone who thinks violence is the only means to clinch into power. Nina mwaka sijachangia blog hii sababu za biaseness, nahisi kuwa post hii isipotoka ntasubiri miaka miwili tena kujaribu ingine
Jamani tuweke ubinadamu mbele kwani mngemwagia maji ya baridi tu si ingetosha mpaka mumharibu kiasi hicho nguvu kazi ya Taifa mdogo kabisa huyo. Uko wapi Ubinadamu wetu Watanzania? Hasira tuzitolee kwenye makaratasi ya kupigia kura na sio kwenye miili ya Watanzania wenzetu.
ReplyDeletePole sana Mussa.
kweli mdau hapo juu tuweni na utuu hata kidogo natuweni na hofu ya mungu jamani mnatupeleka wapi
ReplyDeleteAcha kubisha wewe unayebisha hapo juu, na hayo ni matokeo ya siasa za chuki zinazopandikizwa na viongozi wa Chadema, maana walishawaambia vijana wao kuwa lazima damu imwagike. Na hayo yametokea baada ya mkutano wa Chadema, kila siku kuinstigate terror na kuhamasisha violence.
ReplyDeleteKuna haja kwa mwandishi wa habari kuacha ushabiki unapoandika habari. Unaposema waliommwagia tindikali ni "wafuasi wa CHADEMA" una ushahidi gani? Uliangalia kadi zao za chama? Ulitumia njia gani kujua hilo? Kama huna hakika acha kuandika hisia. Kumbuka vyombo vya habari vinachangia kuleta mitafaruku katika jamii. Sitarajii blog ya jamii ifike huko.
ReplyDeleteIkumbukwe kuwa Mheshimiwa Kubenea alimwagiwa tindikali. Japo ni mambo mawili tofauti lakini mtu anaweza kuuliza, je, na huyu pia alimwagiwa na wafuasi wa CHADEMA? Kama hapana, ni nani? Alitumwa na nani? Je, katumwa na Igunga pia? Hakuna ajuae!
Mi naamini blog ya jamii kama ingandika muswada wa kutoa elimu ya uraia kuhusu uchaguzi hususani Igunga ingapata mfadhili na ingewaambia wana Igunga kuwa hakuna sababu ya kuumizana maana kazi yao ni kupiga kura. Watakaofaidika ni wengine ukizingatia siasa za Tanzania kwa sasa ambapo kuwa kiongozi ni "deal" sio dhamana!
MUNGU ibariki Tanzania,
MUNGU ibariki Igunga na wana-Igunga,
MUNGU ibariki blog ya jamii.
Kikongoti (bkm1209@gmail.com)
WE KIPILI SOMA TAARIFA ILIYOAMBATANA NA PICHA MBONA HAIKUDAIWA KWA VYAMA VINGINE? WEWE KAMA NI MFUASI WA CHADEMA NI KWA NAFASI YAKO LAKINI MADAI NI KUWA WAFUASI WA CHEDEME NA HILO HALINA UBISHI MADARAKA HUWA HAYALAZIMISHWI KWA KUPITIA NJIA KAMA HIZO KWA KILEFU CHADEMA HAMTUFAI HATA KIDOGO MWENDE ZENU MKAFANYE BIASHARA ZENU ZA UJAMBAZI
ReplyDeletewewe anonymous hapo juu hujui lolote ndio maana hata kuandika kiswahili lugha yako ya taifa pia huwezi (Kwa kilefu)maana yake ni nini ulitakiwa uandike kwa kirefu
ReplyDeleteUshauri wa bure rudi shule ukasome
pole tesha! lakini kwanini ccm wabandike mabango ya mgombea wao usiku? mchana walikuwa wanafanya nini? kubandika mchana ni vizuri zaidi, kwani kuna mwanga na hata aliyemwagia angeonekana au ni kufuatana na maelekezo ya "fundi"? inadaiwa CHADEMA ni chama cha kikabila, sasa Tesha anafanyakazi ya kubandika mabango ya pinzani? na CHADEMA wanamwagia tindikali TESHA? mbona naona kizunguzungu!!!
ReplyDelete