Hospitali ya Taifa Muhimbili ilipokea mgonjwa toka Hospitali ya Mwananyamala tarehe 18/08/2011 akiwa mahututi na hajitambui. Inasemekana kuwa mgonjwa huyu aliokotwa na wasamaria wema barabarani akiwa amegonjwa na gari usiku wa kuamkia tarehe 18/08/2011 ambao walimpeleka Hospitali ya Mwananyamala. Kwakuwa alikuwa ameumia sana Hospitali ya Mwananyalama iliamua kumleta Hospitali ya Taifa Muhimbili ili aweze kupata huduma na uchunguzi mkubwa zaidi.


Mgonjwa huyu hajulikani jina lake kwani hawezi kuongea toka alipoletwa kutokea Mwananyamala. Mgonjwa huyu alifanikiwa kuonwa na madaktari bingwa siku hiyohiyo ya tarehe 18/08/2011 na kufanyiwa uchuguzi wa vipimo mbalimbali ikiwemo X-Ray ya tumbo, kichwa, kifua na kiuno. Matokeo ya vipimo hivyo yalionekana kuwa kichwani kulikuwa na damu kidogo iliyoganda kutokana na kuvujia kwa ndani, picha za kifua na kiuno zilionyesha kuwa hakuna tatizo.


Picha ya tumbo ilionyesha kuwa bandama lilipasuka hali iliyopelekea kufanyia upasuaji siku hiyohiyo ya tarehe 18/08/2011 ili kuondoa bandama. Baada ya upasuaji mgonjwa alipelekwa moja kwa moja chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) siku hiyo hiyo ya tarehe 18/08/2011.


HALI YAKE:
Tangu apelekwe ICU hali yake bado ni mbaya, hajitambui. Aidha tangu tarehe 18/08/2011 hakuna ndugu au jamaa aliyejitokeza kuulizia hali ya mgonjwa huyu.
Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili unaomba yeyote anayemfahamu mgonjwa huyu atoe taarifa kwa ndugu na jamaa zake ili waweze kuja kumtambua ndugu yao. Tunaendelea kumpa huduma zote ikiwemo chakula na dawa.


DSC03413.JPG 
DSC03416.JPG
DSC03417.JPG
DSC03419.JPG 
 Imetolewa na:
Aminiel Aligaesha,
Afisa Uhusiano,
Hospitali ya Taifa Muhimbili,
Septemba 2, 2011.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Wataalam, nielimisheni
    Why cant I see these pictures
    There is just one big black square

    ReplyDelete
  2. pole sana mgonjwa na mungu akusaidie.hao ngugu labda hawana taharifa yoyote..labda mngetoa picha za mgonjwa kwenye itv ili zionekane atangwazwe kwenye redio

    ReplyDelete
  3. mbona picha hazionekani?

    ReplyDelete
  4. kwangu mie inanishangaza halafu napatwa na wasiwasi fulani wa kutoamini kitu...mimi mwaka jana mdogo wangu aligongwa na gari na hali yake ikiwa mbaya, alipelekwa mwananyamala na baadae walimrifaa muhimbili...alikaa siku 3 bila kufanyiwa uchunguzi wowote hadi siku ya 4 nilipofika mie nikitokea mbali, nikalipia huduma na ndipo siku hiyohiyo alipofanyiwa uchunguzi...kwa bahati yake mdogo wangu alifariki siku ya 5, sasa nimeshangaa kidogo kusikia kuna mtu aliokotwa amepelekwa mwananyamala na kisha muhimbili HALAFU eti kafanyiwa uchunguzi bila ndugu zake kujulikana au kwa maana nyingine bila malipo ya aina yoyote ile kwa ajili ya uchunguzi?...ilikuwaje kwa mdogo wangu aliyekaa hadi siku ya 4 nilipolipa?...ukweli ni upi we afisa uhusiano!, wataka kuniridhisha kuwa pamoja na mipango ya Mungu lakini kulikuwa na njama fulani hivi za kumuua mdogo wangu kwa vile ni mtoto wa kimaskini au?...maana hadi anafariki kulikuwa na mizengwe mingi sana pale muhimbili kuhusu mdogo wangu...naanza kulazimika kuamini kuwa aliuawa!, na mwenye gari akiwa amepenyeza mkono wake au uwezo wake kwa maana nyingine?...nasema hivi, haki ya mtu haipotei ila inakawizwa tu. kama yupo aliyehusika atalipa tu...no short cut...hadi sasa kesi yake ilivyoisha sijui na malipo toka bima ya gari yamegoma!...eee Mungu tuhurumie sie tusijiweza kwa waovu hawa.

    ReplyDelete
  5. njia iliyo bora nikutoa picha yake ili aweze kutambuliwa ni vigumu kwa maandiko kujua ni nani itakuwa vizuri kuelewa

    ReplyDelete
  6. Matibabu ya muhimu yanatakiwa kuwa bure. Ukitaka matibabu mazuri zaidi na kutokusubiri foleni ndio ulipia sasa inakuwaje watu wasio na uwezo walipia matibabu muhimu? Hii nchi inakwenda pabaya?

    ReplyDelete
  7. Afisa Uhusiano wa Muhimbili inaelekea hujui kazi yako vizuri.
    Umetoa taarifa ndeeefu ya ki-taaluma, yaani "mgonjwa" kafanyiwa x-ray na kachnguzwa bandama etc etc.
    Mbona hujaeleza "mgonjwa" ni jinsia gani? Anakadiriwa kuwa umri gani? Maumbile? Na chochote kile kitakachoweza kumtambulisha? Unatangaza kitu kisicho eleweka, na cha kushangaza hata picha hazijatoka.
    Hii uliitoa awali na nadhani kuna mdau aliyekuuliza maswali haya haya nikuulizayo sasa.
    Jamani fikiria kama vile wewe ndio unaetafuta mtu, je ungetaka information ya aina gani?

    ReplyDelete
  8. Hata usalama wa taifa wameshindwa kutambua jina lake????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...