Wananchi wakishangilia wakati Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Steven Wasira alipokuwa akimtambulisha mgombea wa Ubunge jimbo la Igunga kwa tiketi ya CCM, Dk. Dalaly Kafumu katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kijiji cha Ipumbulya Kata ya Bukoko, Igunga mkoani Tabora, jana.
Vijana wa Ipumbulya kata ya Bukoko wakiomba kwa hamu kushika mkono wa mgombea ubunge jimbo la Igunga kwa tiketi ya CCM, Dk. Dalaly Kafumu, katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika katika kijiji hicho, jana.
Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Dk. Dalaly Kafumu (kushoto) akiwa na familia yake wakati akiitambulisha katika mkutano wa kampeni za CCM jimbo la Igunga, jana katika kijiji cha Ipumbulya, Kata ya Bukoko mkoani Tabora. Anayezungumza ni mkewe, Maria-Magdalena Kafumu na kulia ni watoto wa mgombea, Dk. Lucia Kafumu ambaye ni mganga mkuu hospitali ya wilaya ya Urambo na Benedict Kafumu anayesoma mwaka wa nne udaktari katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hurbert Kairuki Dar es Salaam.
Msanii wa kundi la Tanzania One Theatre (TOT) Khadija Kopa akifanya manjonjo yake,wakati kundi hilo lilipotumbuiza jana katika mkutano wa kampeni za CCM jimbo la Igunga, kwenye Kijiji cha Ipumbulya kata ya Bukoko mkoani Tabora.
Mkazi wa Ipumbulya akiwa amembeba mtoto wake begani apate kumuona mgombea ubunge jimbo la Igunga, Dk. Dalaly Kafumu katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji Kata ya Bukoko jana.
Mkazi wa kijiji cha Ipumbulya Kata ya Bukoko mkoani Tabora Muri Shija, akitazama mfano wa karatasi ya kupigia kura, iliyobandikwa katika kijiji hicho.
Msanii wa kujitegemea Hafsa Kazinja akicheza na 'mchumba' wake John Shigella ambaye alimchagua kucheza naye katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika jana katika kijiji cha Ipumbulya Kata ya Bukoko mkoani Tabora.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM, Asha Abdallah Juma akimwombea kura kwa wananchi mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Dk. Dalaly Kafumu katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika jana katika kijiji cha Ipumbulya Kata ya Bukoko ,jimbo la Igunga mkoani Tabora.Picha zote na Bashir Nkoromo.
dada Hafsa umeshiba kweli.
ReplyDeleteIla michuzi inavyoonekana unawapigia ccm kampeni
ReplyDeleteHuyu mgombea anaonyesha anasikitisha kuomba kura, subiri achaguliwe, hamumuoni tena, anenda kula bata na familia yake. Ukerewe
ReplyDelete