Na Nafisa Madai -Maelezo,Zanzibar
Mwenyekiti wa kamati ya mawasiliano na majenzi ya baraza la uwakilishi makame mbarok mshimba ameitaka mamlaka ya vyombo vya bahari kufuata sheria za mamlaka hiyo kwa kunusuru maisha ya wananchi.
Mshimba ametoa kauli hiyo alipokutana na mamlaka hiyo na waakuu wa kapuni zote za meli zinazochukua abiria na mizigo huko ofisi ya miundombinu na mawasiliano malindi mjini Zanzibar.
Aidha alisema mamlaka pamoja na kampuni za meli lazima zifuate sheria zilizopo na taratibu walizojiwekea na kujifunza na matokea mbalimbali yanayoisababishia taifa kupoteza nguvu kazi zake.
Hata hivyo alisema iwapo sheria za vyombo vya bahari zitafuatwa ajali za meli zinaweza kuepukika,ambapo alisema hivi sasa kampuni zimekua zikicheza na roho za watu.
Sambamba na hayo mhe mshimba aliitaka mamlaka hiyo isitishe safari za usiku mara moja kwani endapo ajali ikitokea asubuhi au mchana uwezekano upo mkubwa wa kuokoa maisha ya watu kwa urahisi.
Aidha alisema ubinafsi kati ya mamlaka ya vyombo vya bahari na wamiliki wa meli usiwepo kati yao kwani kufanya hivyo kutasababisha mizozo ya mara kwa mara isiyo na mantiki katika kazi zao.
Kwa upande wake mkurugenzi wa mamlaka ya vyombo wa bahari Haji Vuai Ussi amesema licha ya kuwa mamlaka yake ni changa lakini kuna sheria ambazo zinaongoza taratibu za mamlaka hiyo bila ya kuingiliwa na mamlaka nyengine.
Aidha alisema mamlaka yake inatoa mashirikiano ya hali ya juu kwa makampuni ya meli,ambapo alisema wamiliki wamekua wakitupia lawama mara kwa mara katika mamlaka hiyo bila ya kutaka kujua sheria za mamlaka hiyo.
Hata hivyo alisema mamlaka yake ina uwezo wa kuzuia meli iwapo meli hiyo itakua haina viwango vya kufanya zoezi la kuchukua abiria na mizigo na hivi karibuni mamlaka itafanya zoezi maalum la ukaguzi wa meli.
Nae mmiliki wa kampuni ya sea star salum turkey sekta ya baharini ina matatizo makubwa ambayo yasipo angaliwa kwa undani wake taifa litapoteza watu wake kila siku.
Akitaja matatizo yanayoikabili sekta hiyo ni pamoja na uchakachuaji wa mafutwa unaofanywa na baadhi ya kampuni ambazo zinazomiliki meli na uuzaji wa mafuta kutokana ushindani wa kibiashara na kulazimika boti yake kulala mara kwa mara.


Kampuni ya Seastar inachekesha kusema kuwa swala la mafuta ndio kikwazo kwao. Sisi wasafiri wa Zanzibar tunajua kuwa Seastar ilikuja na vyombo viwili vipya vizuri sana, lakini kutokana na matatizo ya ununuaji wa vipuri sasa hivi wanaendesha chombo kimoja na chombo hicho kiko taabani, vipuri vinatolewa kama chombo kilicholala na kutiwa humu ili itembee.
ReplyDeleteBwana Turkey hawa watu wengine wenye vyombo baharini mafuta wanapata wapi? Maana tunaona Seagull, Serengeti, Flying Horse, Sea Express, Azam Marine na wengine wanatembea kila siku, basi mafuta hayo yanakuwa mabaya kwa chombo chako wewe tu?
Tafadhalini msitufanye wajinga, sisi wasafiri tunafahamu vizuri sana chombo gani bomu na chombo gani bomba.
Tengenezeni vyombo vyenu viwe katika standard inayokubalika kupakia abiria.
Jambo lingine linalo tukera wasafiri, ni kule kupakia abiria pamoja na mizigo mizito kama meli ya mzigo. Hivi vyombo vya kusafirisha abiria kati ya Dar-es-Salaam na Zanzibar vipakie abiria na vizigo vidogo vya mkononi vya abiria lakini inasikitisha kuwa tunapakiwa abiria na mzigo unafikia kontena mbili kama si tatu katika chombo kilichojengwa mahsusi kwa kupakia abiria. JAMANI WAHUSIKA HILI HAMLIONI?