Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru (kulia) akimkaribisha Waziri wa Afya, Dk Haji Mponda katika hafla ambayo benki hiyo ilikabidhi msaada wa gari la kutolea huduma za tiba linalotembea (mobile clinic) kwa Waziri huyo kwa ajili ya Bodi ya Afya Mkoa wa Dar es Salaam jijini humo leo. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Jerome Ringo na wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecki Sadiki
Waziri wa Afya, Dk Haji Mponda akikabidhi funguo za gari la Mobile Clinic lililotolewa msaada na benki ya NBC kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Afya Mkoa wa Dar es Salaam , Jerome Ringo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecki Sadiki.
Baadhi wa maofisa wa NBC na wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini hafla ya makabidhiano ya gari la Mobile Clinic lililotolewa msaada na benki ya NBC kwa Bodi ya Afya Mkoa wa Dar es Salaam katika Viwanja vya Karimjee jijini humo leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki (kushoto) akifurahi na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru katika hafla ambayo benki hiyo ilikabidhi msaada wa gari la kutolea huduma za tiba
linalotembea (mobile clinic) kwa Waziri wa Afya, Dk Haji Mponda (hayupo pichani) katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Wacheza ngoma wa kikundi cha Makumbusho Cultural Troupe wakitoa burudani katika hafla ya makabidhiano ya gari la Mobile Clinic lililotolewa msaada na benki ya NBC kwa Bodi ya Afya Mkoa wa Dar es Salaam katika Viwanja vysa Karimjee jijini humo leo.
Hivi Mafuru ni mzee au kijana? Huyu jamaa huwa ananichanganya changanya kiaina.
ReplyDelete