Never say never with ATCL
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bw. Paul Chizi (mwenye suti) akiipokea ndege hiyo
Ndege ya aina ya Dash 8-300 ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) iliyokuwa nchini Afrika Kusini kwa muda mrefu kwa matengenezo imerudi nchini juzi jumamosi jioni tayari kuanza kazi.
Ndege hiyo iliyokuwa inaendeshwa na Kapteni Pandya na Kapteni Lila iliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere saa 12.45 jioni na kupokewa na wafanyakzai wa ATCL wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bw. Paul Chizi.
Akiongea na vyombo vya habari uwanjani hapo Bw. Chizi alisema Shirika lake linajipanga kumaliza taratibu muhimu kabla ya kuanza tena safari zake. Alisema iwapo mambo yote yatakuwa yamekamilika kufikia tarehe 25 Septemba mwaka huu, ndege hiyo itaanza safari za kwenda moja kwa moja Kigoma kila siku.
Aliongeza kuwa baada ya muda mfupi, wataanza safari za kwenda Tabora mara nne kwa wiki. Bw. Chizi ambaye ameteuliwa hivi majuzi kuongoza ATCL alisema baada ya mwezi mmoja wataanza safari za kwenda Zanzibar na Arusha.
Kuhusu kuongeza idadi ya ndege, Bw. Chizi alisema kuna Dash 8-300 nyingine ambayo itafanyiwa matengenezo hapa hapa nchini hivi karibuni ili kuokoa pesa na muda. Hata hivyo alifafanua kuwa tayari wameweka mkataba na kampuni ya Jetlink (T) Ltd wa kupata ndege nyingine haraka iwezekanvyo endapo kutakuwa na haja hiyo.
Bw. Chizi aliongeza kuwa ATCL ina mipango ya muda mrefu ya kununua ndege zingine mbili za aina ya CRJ 700 zenye uwezo wa kubeba watu 70 ili kuzidi kuonggeza ubora wa huduma zake.


Ni matumaini yetu hiyo ndege imetengemaa vizuri.. Yasije yakatokea maafa kama ya Zanzibar.
ReplyDeletesijui nisemeje, mie nilikata ticket jan this year-round trip ya dar -mza-dar sasa wakati wa kurudi ndo ndege ikasitishwa huwezi amini sikulipwa wala nini wakasema hadi waanze tena, ikabidi kutafuta nauli ingine ya kunirudisha dar nilikasirika sana basi tu, sasa mtuambie taratibu za kuja kuchukua pesa zetu kwanza kabla ya kuanza kwa hizo safari zenu!
ReplyDeleteNashauri waanzishe na online booking. Mambo ya kwenda pale ATC house na kukutana na wala rushwa wayamalize. Sintosahau mwishoni mwa 2009 nilipofiaka kutaka ticket ya kuelekea kanda ya ziwa nikakuta na collusion ya kufa mtu katika ticket. Ukiwaona wadada wazuri na wengine wamama watu wazima na shungi zao ila balaa. Ananiambia nafasi zimejaa ngoja nimpigie mtu kuuliza, kisha wanaanza kuonge coding language, na kuniambia tarehe ninayotaka ndege haipo labla ingine, akanitajia nikasema poa, akasita kidogo na kuniambia subiri akapiga tena na kuniambia nayo imejaa nimwachie namba ya simu. Kumwachia ananipigia eti kapata nafasi ila nilipe cha juu, nikamwambia basi.
ReplyDeleteWafanyakazi kama hawa ndiyo wanaua shirika, dawa pekee ni kuwa na system ya booking online. Mtu anaingia na ku-book, anapewa ID ambayo atatakiwa ndani ya masaa matatu awe ameiwakilisha kaunta kwa malipo. I kwenye ID hiyo inaprint time ya booking, na akifika kaunta cha kwanza ni kupitisha katika scan ID hiyo ili kuzuia mambo ya umechelewa kapewa mwingine. Utaratibu huu utaifanya ATC kujiendesha kwa faida. Otherwise kama wanaona wafanya wala rushwa wamekaa mezani na visu vyao wakifurahia ndege hii mpya.
Sasa jamani wabook online kwa ndege moja? Hii ni aibu tupu!!!! Yaani after all these years ATCL inaita waandishi wa habari kuja kuona kajindege kalikotengenezwa, mbona hii ni aibu, watu wako proud of upuuzi
ReplyDelete