Na Mwandishi wetu,
Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Bw. Omari Nundu amemteua Bw. Paul T. Chizi (pichani) kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Ndege, ATCL.
Uteuzi huo ulianza tarehe 11 Agosti, 2011 na utaendelea hadi hapo Rais atakapouthibitisha au kuteua mtu mwingine.
Akiongea na mwandishi wa habari hizi jana, Bw. Chizi alisema kazi kubwa iliyoko mbele yake ni kuifufua ATCL.
Hivi sasa ndege za ATCL hazifanyi kazi lakini Bw. Chizi aliahidi kuwa ndege zitaanza kuruka hivi karibuni. Hakutaka kutoa maelezo zaidi akisema ni mapema mno kutoa mikakati iliyopo.
Bw. Chizi ni Mhandisi wa ndege mwenye uzoefu wa siku nyingi. Ana Shahada ya Uzamili ya M.sc kutoka chuo cha Odessa Polytechnic katika Soviet Union. Pia ana shahada ya Uzamili ya MBA kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM).
Alijiunga na lililokuwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATC) mwaka 1979 kama Injinia wa Mipango na Matengenezo na akapanda hadi kufikia Unaibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika mwaka 2002.
Chizi alistaafu kwa hiari 2002, na kuanzisha Kampuni yake ya kutoa ushauri inayoitwa Customer Support Systems Ltd. Ametoa ushauri wa kitaalam kwa mashirika yapatayo 60 (sitini) hapa nchini na nje ya nchi.
Kutoka 2007 hadi 2008 alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Community Airlines. Kutoka Machi, 2011 hadi alipoteuliwa na Waziri Nundu alikuwa Meneja Mkuu wa Jetlink Express (T) Ltd.
Bw. Chizi ana umri wa miaka 58, ameoa na ana watoto watano.
Jamani lakini hili sio Shirika la umma tena kama mnavyoonyesha kwenye habari hapo.
ReplyDeleteHii ni Limited Company iliyosajiliwa chini ya Sheria ya Makampuni Sura 212.
Sasa the Companies Act inaruhusu utaratibu huo wa kuchaguana wakurugenzi kienyeji hivyo au wanateuliwa kwenye MEMBERS(SHAREHOLDERS) MEETING au ANNUAL GENERAL MEETING.
AG yuko wapi? anashindwa kushauri hilo.
Wenye ujuzi zaidi wa Company Laws hebu tuhabarisheni
Hongera Kwa Uteuzi. Una kazi Nzito Mheshimiwa wa kupeperusha Flag Carrier
ReplyDeleteLabda huyu atatuvusha
ReplyDeletelets wait n c
He he he heeee Chizi kapewa rungu!
ReplyDeleteHili dubwashika linahitaji mtu 'chizi' kwelikweli, no pun intended!
ReplyDeletewadau pole pole jamani acheni uchizi
ReplyDeletehuyu chizi naona analijua shirika nje ndani kwa hiyo tutarajie habari njema