Mtanzania anayecheza Soka ya kulipwa katika timu ya White Caps ya jijini Vancouver Canada,Nizar Khalfan akimkabidhi Rais Dkt. Jakaya Kikwete jezi ya timu yake wakati alipokwenda kumsalimu na kumshukuru kwa mengi aliyofanya katika kufufua na kuendeleza michezo na wachezaji Ikulu jijini Dar es Salaam leo jioni.(picha na Freddy Maro)
Home
Unlabelled
Nizar Khalfan amkabidhi jezi Rais Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
alikwenda kumtembelea na kumshukuru!...alikwenda kumshukuru nini?
ReplyDeleteAnamshukuru kwa kumleta Maximo wewe, bila Maximo watu wasingeonekana....
ReplyDeleteJamani Ikulu ngoja na mimi nijipange kwenda, sasa sijui nitasema ninacheza mchezo upi!!! Lkn Mhe. amejitahidi sana kuwaweka wananchi wake karibu na Ikulu yao ila wanamichezo wamezidi. Kulikoni? Wachumi vipi?
ReplyDeletegood question and as they say thanks for nothing.a bunch of crap.
ReplyDeleteKaenda kumchomea babu, anasema bora Maximo
ReplyDeleteMaamuzi magumu yanasubiri. Hivi mkuu wa Mkoa wa Dar ni nani?
ReplyDeleteAnamshukuru JK kwa kumleta Maximo na kumsaidia kuonekana...crap! Mi nadhani JK anapaswa kufanya ziara za mikoani sasa kuliko kushughulikia masuala ya namna hii. Nenda Shinyanga, Rukwa n.k. kakague miradi na kuwaeleza wananchi serikali yao itawasaidia vipi kukabiliana na njaa ya mwaka huu.
ReplyDeletemimi nazani serekali wangefungua ka ikulu ndogo cha mikutano, ambayo raisi anaweza kukutana na yoyote hatakaye kwenda kumshukuru!
ReplyDeletemdau kenya
Ehe! nami ngoja nijipange kwenda ikulu....... labda mie niende kutazama siri za kuandika wiki leaks maana naona ni rahisi sana kuandika hata uwongo. Si nitajulikana nilikwenda ikulu?
ReplyDeleteMnaotaka kwenda mjue kama unataka kwenda kujadili mada muhimu kama Kuepukana na mgao wa umeme , jinsi ya kufufua uchumi na kuongeza makusanyo ya kodi , na mengine yanayofanana na hayo mjue kabisa hamna nafasi
ReplyDeletebado hamjakoma tu? hashim si mlimkaribisha hivyo hivyo? leo hii hayuko tena NBA (poor thang) sasa huyu kinachofuata nini?? chakula cha usiku? lakini ukiweka utani nyuma huyu kijana ni ana kipaji kweli, mi nilimwona anavyocheza, tuombe mungu tu atuletee KOMBE
ReplyDeletekwanini hilo shati lisingekuwa na jina lake yeye mwenyewe mchezaji kama wachezaji wote wanavyofanya?? huyu kaka nani kamshauri hivyo? lakini ngoja tumpe muda labda atatujengea jina zuri huku canada
ReplyDeletewaswahili acheni majungu na wivu mtu basi asipate chansi huku ulaya?? ila tatizo wengi wakipata fursa ya kuwa chumba kimoja na JK wanajisahau basi hapo trip za bongo zitakuwa kila siku na ndio hapo atakapomalizikia, tuombe mungu huyu abakie huku kwa muda mpaka jina lake liote mizizi ndio awe anarudi rudi nyumbani kufanya vitu vyake.
ReplyDeleteKWA MAWAZO HAYO MLIYONAYO WATANZANIA KWA KWELI HATUTAENDELEA. KIONGOZI LAZIMA AWE KARIBU NA WATU WAKE. ALIENDA KUMSALIM RAIS NA KUMPA UZOEFU WA KIMICHEZO TOKA KWA WENZETU HUKO MAJUU. ACHENI SIASA JAMANI!
ReplyDeleteUuuuuuiiiiiiiiiiii wajemeni hebu acheni wivu wakijinga.Kila kiongozi anastaili yake ya kuiongoza nchi.Anayo haki zote za kukaribisha mtu yeyote yule na kama ni kinyume na sheria basi nendeni mkamshitaki.Heeeee!!! mara mseme kazidi kukaribisha wananmichezo,mara kazidi kufutarisha mara sijui nini wacheni tabia zenu mbaya na roho za kwanini.
ReplyDeleteKelele za sakafuni hazimkatazi mwenye Nyumba kulala. Semeni Semeni......hii nyimbo mnaijua. Kikwete hangoki mpaka 2015. Maandamano mbona hamkufanya. Slaa mbona kimya siku hizi au babu machokumchuzi kamweka plasta.
ReplyDeletekwani mmeambiwa ikulu ni mbinguni watu hawawezi kwenda?
ReplyDeleteNawe unayesema aende mikoani hao wakuu wa mikoa na wilaya wanafanya kazi gani?
Akiwa yuko Ikulu ooh safiri, akisafiri ooh Vasco da gama. kweli ubinadamu kaazi hasa ukiwa mbongo!!