Ndugu zangu,
Ndani ya siku tatu za kupiga kura kwenye Pima-Maji ya Mjengwablog, watu 165 wameshatumbukiza kura zao. Matokeo mpaka dakika hii ni Joseph Kashindye wa CHADEMA anayeongoza kwa kura 116 akiwa amejinyakulia asilimia 70 ya kura zote. Anayefutia ni Dr. Peter Kafumu wa CCM mwenye kura 39 sawa na asilimia 23 ya kura zote. Wa tatu ni Leopard Mahona wa CUF mwenye kura 10 sawa na asilimia 6 ya kura zote.
Tafsiri yangu;
Huu utakuwa mpambano mgumu mpaka dakika ya mwisho. Kwamba leo Jumanne wagombea wa vyama saba vya upinzani wamerudisha fomu si habari njema kwa CHADEMA. Tayari katika hatua hii ya kura za maoni za Watanzania wa mtandaoni tunaona CUF kwa namna moja au nyingine imepunguza kura za CHADEMA kwa asimilia 6.
Laiti CUF na vyama vingine vya upinzani vingeiachia CHADEMA ipambane na CCM na huku vyama hivyo vikiipa sapoti CHADEMA, basi, CCM wangekuwa na kibarua kigumu zaidi kulibakisha jimbo la Igunga mikononi mwake.
Na kama mgombea wa CHADEMA atabaki kwenye asilimia 60 au 70 ya ushindi siku tatu kabla ya uchaguzi, basi, Peter Kafumu wa CCM anaweza kabisa kuapishwa kuwa Mbunge wa Igunga kwenye Bunge la Kumi na Moja mwezi Novemba. Kwanini? CCM ni mabingwa wa ' kuokoteza' kura kwenye siku za mwisho za kampeni, kwa mbinu zote. Hivyo basi, kumfanya mgombea wao aibuke kidedea.
Na Siku tatu zijazo zitatoa picha zaidi juu ya hali ilivyo kwenye uwanja wa mapambano ya kisiasa kule Igunga. CHADEMA watazindua rasmi kampeni zao, alikadhalika CCM na CUF. Hotuba za uzinduzi na mwitikio wa Wana Igunga kwa kila chama kitapozindua kampeni zake unaweza kutusaidia kutafsiri mwelekeo.
Naingiwa na hofu. Kwanini?
Kuwa Igunga inaweza pia kuwa kwenye hatari ya vurugu za kisiasa kama zilizotokea Tarime. Ni kwa vile CCM, CHADEMA na CUF vyote vimeikamia Igunga. Na itangulizwe busara na maslahi ya taifa.
Msomaji unakumbushwa. Nini tena?
Kuwa Pima-Maji ya Mjengwablog juu ya kinyang'anyiro cha Igunga bado inaendelea. Itumie blogu yako ya jamii shirikishwa ili utoe maoni yako. Zimebaki siku tatu za kupiga kura kabla kituo cha kupigia kura kufungwa. Piga kura yako sasa hapo juu kulia. Na kisha angalia matokeo. Kumbuka, kompyuta moja, kura moja. Ndio, hii ni Pima-Maji isiyochakachulika!
Maggid,
Dodoma.
MNAJIFURAHISHA TU! IGUNGA NI SISI NA SISI NI IGUNGA. KUFURUKUTA MTAFURUKUTA LAKINI HAKUNA WA KUCHUKUA JIMBO LA IGUNGA ZAIDI YA CCM. MAJID ATAKUWA AMEPIGA KURA YEYE MWENYEWE NA MARAFIKI ZAKE WANAOSAPOTI CHADEMA.
ReplyDeleteWAPIGA KURA WETU BADO WANA IMANI NA CHAMA CHAO PAMOJA NA MISUKOSUKO TUNAYOIPATA.
CCM NI NO.1 WENGINE MNAJIKONGOJA.
Tafsiri yangu ni kwamba wanachama asilimia 30 ya wana CHADEMA wamewapigia kura wagombea wasio wa CHADEMA. Na Maggid huna sifa za kuendesha maoni huru, kwani ulichoandika hapo juu kinaonyesha wazi unaegemea wapi na una nia gani. Kwa nini CUF waunge mkono Chadema na sio Chadema waunge mkono CUF? Hivi unaweza kutuambia kwamba ni watoa maoni wangapi hapa wana sifa za kupiga kura Igunga? Acha uchochezi kijana!
ReplyDeleteKyadema watake wasitake, WanaIgunga tutampigia kura Dr P Kafumu wa CCM na atapata ushindi mkubwa sana sana. Copy and paste that. CCM IMARA DAIMA. MwanaIgunga menyu.
ReplyDeleteAnkal tafadhali mwambie ndugu yetu Mjengwa kuwa hiyo kura yake ya maoni haiakisi hali halisi ya Igunga kwa sababu moja tu: Katika uchaguzi wa ubunge Igunga watakaopiga kura ni wananchi wa Igunga NA SIYO NDUGU ZAKE GODBLESS LEMA NA FREEMAN MBOWE WALIOPIGA KURA KATIKA PIMA-MAJI YA Mwenyekiti M Mjengwa katika mjengwa.blogspot.com. Namheshimu sana Maggid Mjengwa na ninamshauri kama anataka kuja hali halisi na matakwa ya wapiga kura wa Igunga basi aje hapa Igunga ambako tutamkaribisha kwa mikono miwili badala ya kutegemea "maoni" ya hao ndugu zetu wa mkoa fulani wa kaskazini. Ahsanteni.
ReplyDeletesi kweli hizo kura za maoni zimetumika kwa mtindo gani?nadhani pia asilimia kubwa ni watu wa mjini ndio wamechagua na sio wahusika wa igunga.pia nyie waandishi ndio mnaleta mtafaruku na sio wanachma.jirekebisheni hii inchi ni ya amani.unatoa kura za maoni zisizonahusiano na wapiga kura wa igunga alafu matokeo yakitoka.waseme wameibiwa.naipenda tanzania na watu wake
ReplyDeleteJidanganyeni tu! Mnafikiri wana Igunga bado tumelala eeeeeeeh? Uzuri mtajionea wenyewe. Muwe tayari kuyakubali tu matokea msije mkatumia maji ya upupu. Maisha magumu kwa kila mtanzania hatuyataki.
ReplyDeleteMjengwa unajidanganya na pima maji yako. wanaopiga kura ya maoni ni watu wa mjini wenye access ya internet ambao sio wapiga kura wala wakazi wa igunga. Je unaweza kuniambia asilimia ngapi ya watu wana access na uwezowa kutumia internet/computer?. Siipendi CCM lakini ukweli utakuwa na kampeni kali kwa vyama vitatu, CCM,Chadema na CUF, mwisho wa siku CCCM itashinda kwa kishindo. Inasikitisha mwandishi makini kama wewe unashindwa kuchambua kwa makini hali halisi ya IGUNGA kwa sasa.Pole na tafakari
ReplyDeleteUpinzani wakitaka kushinda itawalazimu wafanye kazi ya ziada.
ReplyDeleteWapigakura wasiojua kusoma na kuandika, wapenda kofia, khanga na T-shirt za CCM na wapenda kununuliwa pombe ni mtaji mkubwa wa CCM.Pia waweke mawakala waaminifu kila kituo cha kupigia kura. Wakiyazingatia hayo, Chadema au CUF watashinda. CCM imepoteza dira japo bado inajua vema jinsi ya kupata kura.
Mimi si mwanaIgunga wala Mdanganyika lakini Igunga mimi ninavyoiona, watu wametoa machozi pale Rostam alipotangaza kuondoka pamoja na matope yote mliyompaka, hivi wewe Mjengwa una akili nzuri na unafikiri watu wote WADANGANYIKA. Nyinyi kweli watoto katika siasa. Kule pemba wana shida kama nini CCM wanamimina mapesa na misaada kem kem, kura zote wanapewa CUF. Hizo kura obviously wamepiga hivi vifaranga vya siasa vilivyodumaa vilivyojaa upupu katika aini (macho) zao. INASIKITISHA MWANDISHI MWANDAMIZI KAMA WEWE UNAJITIA AIBU KAMA HIVI. VERY POOR ANALYSIS.
ReplyDeleteUseless! matokeo yanaonesha Chadema wanaongoze lakini mwandishi anasema mwisho wa siku CCM itaibuka mshindi!
ReplyDelete