Na Hassan Mtengefu, wa Jeshi la Polisi Rukwa.

Jeshi la Polisi mkoani Rukwa limetoa ufafanuzi juu ya taarifa zilizoandikwa na gazeti moja linalotolewa kila siku kwa lugha ya Kiswahili katika toleo lake la Septemba 01, mwaka huu lenye kichwa cha habari “POLISI MPANDA LAWAMANI, Ni Kwa Kumlinda Mlalamikiwa”.

Kamanda wa Polisi mkoani humo SACP Isuto Mantage, amesema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote na kwamba Mwandishi wa Habari hizo mbali ya kuwa hakufanya utafiti wa kutosha pia aliupotosha umma na alikuwa na nia ya kulidhalilisha Jeshi la Polisi na watendaji wake.

Kamanda Mantage amesema kuwa ukweli wa taarifa hiyo ni kuwa mnamo Julai 2, 2011 majira ya saa 9.00 alasiri Kituo cha Polisi Mpanda kilipokea taarifa kutoka kwa mkazi mmoja wa eneo la Kawanjese mjini Mpanda,Bi. Justin John kuwa siku hiyo majira ya saa 8.00 mchana mtoto wake Angel Daudi, mwenye umri wa miaka miwili na miezi saba, alibakwa na kijana mmoja aitwaye Maneno Hassan kisha kukimbia.

Baada ya taarifa hizo, Polisi walifanya juhudi za kumsaka mtuhumiwa na kumkamata na baada ya mahojiano ilibainika kuwa kijana huyo Maneno Hassan (16) alikuwa ni mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Muungano iliyopo mjini Mpanda.

Polisi walifanya upelelezi wa haraka na Julay 6, 2011 walimpeleka mtuhumiwa huyo katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda na kufunguliwa kesi CC (Criminal Case) namba 163/2011.

Kesi hiyo ilifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mh. ROBERT KASELE – DRM na Mwendesha Mashtaka wa Polisi Inspekta Timoth Nyinka, alimsomea mtuhumiwa shitaka lake ambapo alikanusha kutenda kosa hilo.

Mahakama iliamuru mtuhumiwa huyo ajidhamini mwenyewe (Self Bail) na kesi yake ilipangwa kutajwa tena Julai 20, 2011 na kwa vile upelelezi wa kesi hiyo ulikwisha kamilika iliingia katika hatua ya kusikilizwa kwa awali ambapo ilipangwa kwa P/HG Agosti 29, 2011 na ilipofika siku hiyo Hakimu wa kesi hiyo hakufika Mahakamani na kuahirishwa tena kwa kesi hiyo hadi Septemba 21, 2011 ambapo pia hakimu hakuwepo na imepangwa tena kufanyika Oktoba 10, mwaka huu.

Kutokana na taarifa hiyo, Jeshi la Polisi mkoani Rukwa pamoja na kutoa ufafanuzi juu ya tukio hilo, pia limesema taarifa hiyo haikuwa ya kweli "sio kweli kuwa kesi hiyo ilikuwa imemalizwa kituo cha Polisi Mpanda na wala baba wa mtoto aliyebakwa hakupigwa danadana na Polisi kama ilivyodaiwa katika gazeti hilo"alisema Kamanda Mantage.

Jeshi la Polisi limesema kuwa tuhuma hizo zilikuwa na lengo la kulichafua Jeshi la Polisi na Gazeti hilo linapaswa kuomba radhi kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa kwa kuchapisha habari zisizo na ukweli.

Hata hivyo Kamanda Mantage amesema kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na Waandishi wa Habari katika juhudi zake za kuwaelimisha wananchi juu ya mambo mbalimbali yanayotokea na kuonya juu ya matumizi mabaya ya kalamu za baadhi ya Wanahabari wanaoupotosha umma badala ya kuwaeleza ukweli wa mambo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Huyo hakimu kwanini anakosekana mahakamani mara 2 mfululizo! Hivi kesi kubwa kama hiyo ya kubaka/kunajisi kumbe mtuhumiwa anaweza kupewa dhamana! Tena ya kujidhamini mwenyewe! Si ndo akipatikana na hatia anafungwa miaka 30!? Hiyo sio sababu tosha ya kuelewa kwamba akipewa dhamana ata-'sepa'?

    ReplyDelete
  2. Anon1, bila shaka hayo ni maoni yako kuhusu mahakama! Mara nyingi polisi wamekuwa wakitupiwa lawama kwa utendaji mbovu wa mahakama. Kwa kweli inakatisha tamaa sana, hata kama wewe ni polisi, kesi inakuja, unafanya haraka kumtafuta mtuhumiwa na kukamilisha upelelezi. Unampeleka mahakamani, matokeo yake ndiyo hayo! Hakimu hayupo, hayupo! dhamana huru...Mtoto mwenyewe aliyebakwa ni miaka miwili!

    ReplyDelete
  3. Jeshi pia liache kumdhalilisha mtoto kwa kumuweka jina lake hadharani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...