Muasisi na Mwenyekiti wa Bodi wa Precision Air Bw. Michael Shirima (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi wa shillingi milioni 10 Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kama rambi rambi kwa familia za wafiwa na waliookolewa katika ajali ya meli iliyotokea Zanzibar mapema mwezi huu.
Muasisi na Mwenyekiti wa Bodi wa Precision Air Bw. Michael Shirima akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipotembelea ofisi za Makamu wa Rais huyo asubuhi ya leo (jana).
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Iddi (watatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Precision Air. Kutoka kushoto ni Msimamizi wa Mauzo Zanzibar Laurian Joseph, Afisa Mawasiliano Amani Nkurlu, Meneja Mauzo wa Zanzibar na Dsm Nancy Bagaka, Muasisi na Mwenyekiti wa Bodi Michael Shirima, Mkurugenzi wa Biashara Phil Mwakitawa na Meneja wa Uwanja wa Ndege kwa Precision Air Michael Montana.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...