Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimfariji mtoto Said Gerald aliyelazwa katika hospitali ya Mnazi mmoja Zanzibar baada ya kunusurika katika ajali ya meli iliyotokea Unguja juzi usiku.Aliyempakata mtoto Said ni mama yake mdogo Mariam Hemed.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(watatu kushoto) akiwa pamoja na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein(wane kushoto),Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Seif Shariff Hamad(kulia), Waziri wan chi ofisi ya makamu wa kwanza wa Rais anayeshughulikia maafa na muungano, Mohamed Abood Mohamed pamoja Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume wakiwa katika viwanja vya Maisara Unguja kukagua shuguli za kushugulikia miili iliyoopolewa pamoja na kuwafariji wafiwa baada ya kuzama kwa meli huko Unguja juzi usiku(picha na Freddy Maro).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hivi miili ya marehemu inashughulikiwa?

    ReplyDelete
  2. Jamani kiswahili kinapotoshwa. Wahanga ni watu waliojitolea mhanga kufa.Hawa sio wahanga hawa ni watu walionusurika kufa/majeruhi wa kwenye ajali hii ya meli. Michuzi hebu rekebisha.

    ReplyDelete
  3. Mdau wa kwanza "Waheshimiwa walikuwa wanakagua shughuli za kushughulikia miili". Soma kwa makini kabla hujakosoa. Jibu kwa swali lako ni- Ndiyo, miili inashughulikiwa. Kabla ya mazishi inahitaji kuhifahiwa kwa heshima zote zinazostahili. Lazima ziwe safi, zisiharibike, na pia huenda baadhi kusafirishwa, nk. Hizi zote ni shughuri. Usiwe mwepesi wa kukosoa au kusemasema. Mdau wa pili wewe pia unaweza kumezea siku mojamoja. Tutashukuru ukianzisha blog yako isiyo na makosa. Kumbukeni Michuzi anapokea mamia ya email kila siku, nae ni binadamu kuchoka ni kawaida.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...