Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika mkutano huo.

Na Mindi Kasiga,Virginia-Marekani.

Watanzania waishio Marekani wameaswa wasibweteke na badala yake watumie fursa zinazotolewa na serikali ili kupeleka maendeleo nyumbani. Hayo yamesemwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tatu wa Baraza la Watanzania Waishio Marekani leo mjini Dulles, Virginia na Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwenye hutuba yake ya ufunguzi, Rais Kikwete aliwaambia Watanzania kuwa kila mmoja anawajibu wa kusaidia kusukuma gurudumu la maendelo nchini Tanzania kwani ni wajibu wa kila Mtanzania na si Serikali peke yake.

Aidha Rais Kikwete aliwaasa Watanzania wawe ni mfano wa kuigwa na mataifa mengine wakiwa ugenini. Wawe Raia wazuri nchini Marekani, watii wa sheria, wasaidie kusomesha ndugu zao nyumbani ili mafanikio waliyoyapata kwa kuishi ughaibuni, yafike hadi kijijini walipotokea kwa kuwasaidia wale waliowaacha.

Pia Rais Kikwetealiwasisitiza Watanzania walio nje kuwa kamwe wasisahau walipotoka, nyumbani, ikiwezekana waanze kutafuta ardhi na kujenga nyumba za kuishi Tanzania.

“Badala ya kulalamika tu na kuandika kwenye blogs, ni wakati sasa muanze kusaidia kuwekeza nyumbani, kwani nchi ni yetu sote, hakuna mliyemkabidhi alete maendeleo ili yakishapatikana ndio mrudi nyumbani” alifafanua Rais Kikwete huku akishangiliwa na umati wa watanzania uliofurika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Marriot.

Naye Waziri mwenye dhamana ya kuratibu masuala ya Watanzania waishio ughaibuni, Mheshimiwa Bernard Membe, alisema Rais Kikwete ana nia ya dhati, kusaidiana na Watanzania nje ya nchi ili kuhakikisha maendeleo yao yanawanufaisha wao pamoja na Tanzania.

Akisisitiza jitihada za serikali na za Rais Kikwete katika kuhalalisha suala la uraia pacha, ambalo ni mojawapo ya kilio kikubwa cha Watanzania waishio ughaibuni, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alisema ingawa ni suala la kikatiba, lakini Serikali inategemea kuwa ndani ya kipindi hiki ambapo katiba inapitiwa na kufanyiwa mabadiliko, ndio wakati muafaka wa suala hili kujadiliwa kwa kina ili likamilishwe na kuingia kwenye katiba mpya.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na mabalozi wa Tanzania nchini Marekani Balozi Mwanaidi Maajar na Balozi Ombeni Sefue ambao nao walizungumzia sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara wakisema Watanzania wana kila sababu ya kuringa kwani mafanikio ya miaka 50 ni ya kujivunia.

Mkutano huo wa siku tatu uliodhaminiwa na makampuni ya kitanzania tu, umevutia Watanzania zaidi ya 500 kutoka pande mbalimbali za Marekani, na unatarajiwa kujadili njia za kukabiliana na changamoto za wana diaspora ili kuchangia maendeleo na kukuza pato la nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Kikwete akusanye kodi na kupunguza mishahara ya mawaziri na wabunge. Pia komesha rushwa na acha kuwaomba Watz wa nje wakusaidie kwani wao wanasaidia ndugu zao tu na hawana mamlaka yoyote na maamuzi yoyote. Kikwete wewe ndio captain na nchi ina potential kubwa sana lakini umelala usingizi mzito toka uchaguliwe.

    ReplyDelete
  2. tukileta maendeleo yenyewe full ubabaishaji TRA wananyanyasa kinoma utakuta kitu ni cha halali lakini unazungushwa weee hadi unakoma!

    ReplyDelete
  3. Afashali Mr president uwaambie hao jamaa. Wasifikiri kwamba wao wamefika huko waliko wakasahau kwao. Hata wazungu walikuwa na uwezo wa kuishi nchi za wenzao lakini kwa uzalendo wao walirudisha kwenye nchi zao kile walichopata kutoka nchi zingine.

    ReplyDelete
  4. Tatizo ni kwamba Tukipeleka maendeleo nyumbani ndugu zetu wanalewa mapesa tunayowapa bure na kuukwaa UKIMWI. "Easy Come.. Easy Go"

    Sasa ni bora tusubiri kwanza wafunguke macho kwa kuangalia hali ya dunia ilivyo kupitia internet zinazo endelea kuenea kwa siku za hivi karibuni.

    Pia baba zetu wajifunze kutulia na mke mmoja na pia wazae mtoto mmoja au wawili kisha wa-save pesa nyingi za kuwasomesha mpaka chuo kikuu na siyo kuzaa zaa watoto kibao kwa akili za kizamani kuwa kila mtoto anakuja na bahati yake.

    ReplyDelete
  5. kumbe muheshimiwa anasoma blogs anaona wabongo wanavyolalamika heheheheh mithupu mheshimiwa anasoma blog yako , kuwa makini

    ReplyDelete
  6. Mheshimiwa Rais Dk.J.K
    Asante sana kwa kutuamsha,watanzania wengi tunaishi marekani na nje ya nchi kwa ujumla tunajitaidi sana kupereka maendeleo nyumbani,lakini tunakwamishwa na burocrat na mizengwe za baadhi ya watumishi wa idara za serikali nyumbani,zikiwemo TRA,pia maafisa Ardhi,na watendeji wa ngazi za mikoa na wilaya,wamekuwa wasumbufu sana sana,kama sisi watanzania tulio nje tunataka kufungua miradi fulani kwa manufaa ya wananchi hadi kupata kibali au idhini ya miradi hiyo itachukua miaka 10, na bila mafanikio,tunachokuomba ni ushirikiano wako ,uwambie waliokuzunguka na watumishi wa serikali watuchukulie sisi ni wenzao na kututendea haki

    ReplyDelete
  7. Ni huyu huyu Rais amebadilika tena na kusema watu warudi kwao na alipoulizwa swala la uraia pacha alipotembelea California Sillicon Valley ninamnukuu alisema "Watanzania mliokaa nje hamna haja ya kurudi nchini kwenu mkae hukuhuku" Naona sasa anakigeugeu! hapa simwelewi. Watu washio nje ya nchi tumejitahidi kubadilisha maisha ya familia zetu tanzania sio kwamba tumejisahau tunafanya kazi kwa bidii na sio lelemama. Kama tukirudi tanzania na kupewa nafasi ya kulitumikia taifa letu kama tunavyolitumikia taifa lingine hakika tanzania kutakuwa na maendeleo na displine makazini. Tatizo kubwa tunapotuma vitu nchini tanzania kuna urasimu mkubwa sana bado rushwa ni tatizo kwani Rushwa imekuwa sehemu ya huduma ya mtanzania! hata kufungua account ya tanzanite ili ushughulikiwe ni lazima utoe kitu kidogo. Kingine kinachokatisha tamaa ni urasimu. Kufungua account bank ni mpaka upitie process nyingi zisizonamaana zinachelewesha maendeleo na hii ni huwezi kumtambua mtanzania kwani hana utambulisho. Vitambulisho vya taifa ni vya lazima na muhimu kwa kila mtanzania ili kurahisisha kumtambua na kumhudumia mtanzania. Haya ndo maoni yangu kwa leo.
    Mdau USA

    ReplyDelete
  8. Hili suala la uraia pacha lina utata sana, na inabidi litafakariwe kwa makini. Kila nchi ina sheria na taratibu zake kuhusu suala hilo.

    Huu mkutano wa DICOTA umefanyiwa Marekani, nami napenda kusema moja mawili nikizingatia hilo. Mtu anapochukua uraia wa Marekani, anakula kiapo, na kati ya mambo ya kiapo hiki ni kuukana uraia wa nchi anakotoka na kukana kuyatambua mamlaka ya rais na serikali ya nchi ile. Yaani kama mimi nikichukua uraia wa Marekani, naapa kuwa siyatambui mamlaka ya rais wa Tanzania wala serikali ya Tanzania juu yangu. Wadau napenda kuwasilisha suala hili ili litafakariwe.

    Sio kila nchi ina sheria kama hii ya Marekani kuhusu suala hilo. Kwa kiasi nilichoweza kufuatilia, nchi zingine sheria zao hazina utata kama hii sheria ya Marekani, yaani mtu akichukua uraia wao, hategemewi kuukana uraia au mamlaka ya rais na serikali ya kule anakotoka.

    Serikali ya Tanzania inapotoa ahadi kuhusu kuruhusiwa kwa hili suala la uraia pacha ingepaswa ifafanue zaidi masuala tata kama hili suala la kuchukua uraia wa Marekani. Au je, tunatakiwa kulifumbia macho?

    Marekani yenyewe haipendelei raia wake wachukue uraia wa nchi zingine. Hatuhitaji kubishana kuhusu suala hilo. Yeyote anaweza kwenda mtandaoni kwenye tovuti husika akaona sheria na taratibu za Marekani zikoje.

    Napenda kurudia kuwa hapa nimegusia tu kipengele kinachohusu Marekani. Sijagusia vipengele vingine, ambavyo ni vingi.

    ReplyDelete
  9. Muheshimiwa Rais wetu Dr.JK,
    Sisi tunasaidia ndugu na familia.Kuhusu inchi nzima maendeleo yake yanategemea kila mtu na serikali kuwa na policies zinazoweza kulinda na kunufaisha wanainchi wake sio hao walafi.

    Hilo ni tatizo la kusaidia ndugu na jamaa home.
    1. Nimeproduce more lazy people than kabla sijaanza kusaidia.
    2. Ninajenga lakini nimeonga mpaka makamasi yananitoka.
    3. Natuma expensive products huko lakini sometimes vinaibiwa vikifika huko.

    Ni hayo machache,
    David

    ReplyDelete
  10. Hivi ni kweli unataka msaada au utani? sukari miwa tunalima ss ila bei ni sawa na almasi, nyama kula tz now ni mpaka kuwe na sherehe na ng'ombe tunao. Wewe umetulia zako kimya hata kuongea kwa sauti usikike hakuna.Petrol tatizo bado hata ku encourage wananchi hakuna. Tukituma vitu TRA wezi narudia tena TRA WEEEEEEEEEEEZI wala rushwa hata mabagi wanafungua na kuchukua vitu. Hivi hakuna CCTV TRA? Ushuru mkubwa hadi tunakoma, mnacharge kodi kubwa na still maendeleo hakuna hata barabara zimekushinda tangu tumepata uhuru 50 yrs ago kuna wananchi hata maji ya kunywa wanakunywa machafu tena yananuka kila mara wazungu wankusaidia ila nao mnawachaji ghali, Kuna vitu vingine unapaswa kuwapa wananchi wako bure kutokana na umaskini, uzee, ulemavu n.k. But huwapi haki kwanza akiwa mlemavu ndo uonevu unazidi, halafu mnategemea msaidiwe tukituma laptop zisaidie wanafunzi mashule zinaibiwa TRA?PoSTA na unajua watumishi wa umma wanakuangusha ila hujawaonyeshaga mfano wa kumuadhibu hata mmoja tu. Imarisha pale TRA uone kama hujaendelea na kupata kura zingine.

    ReplyDelete
  11. wewe unayesema huko america watu wakichukua uraia wa huko wana takiwa kuapa kuwa wanaikana nchi yao na hawaitambui mamlaka ya raisi wa nchi zao ni uongo. nina marafiki kutoka nigeria, england, namibia na canada ambao wamechukua uraia wa america na hakuna hata mmoja alifanya hivyo. may be hizo laws zilikuweko before. ebu tafadhali google uone ni nchi gani zinaruhusiwa kuwa na dual citizenship in america. canada hawajali una uraia wa nchi ngapi, bado wanakupa uraia wao kama una qualify na huna haja ya kukataa uraia wa nchi uliyotoka. wewe kama huwezi kupata uraia wa america jinyamazie. watu wengi wanafikiri kuwa kila mwafrica aliye america alitumia panya routes kuja huku lakini kuna wengi walikuja kihalali. mimi na mume wangu tulipata work permits kwa kuapply kazi kwenye under servesed areas. tulifanya kazi huko kwa two years ndio tukapewa green cards na tukaweza ku move to washington. kenya sasa inaruhusu dual citizenship kwahiyo hakuna matata.

    ReplyDelete
  12. Anonymous wa Septemba 25, 12:31, ingekuwa vema ungejikita katika hoja iliyopo. Kiapo wanachoapa wanaochukua uraia wa Marekani, ambacho kinaitwa "The United States Oath of Allegiance," ni hiki hapa:

    I hereby declare, on oath, that I absolutely and entirely renounce and abjure all allegiance and fidelity to any foreign prince, potentate, state, or sovereignty of whom or which I have heretofore been a subject or citizen; that I will support and defend the Constitution and laws of the United States of America against all enemies, foreign and domestic; that I will bear true faith and allegiance to the same; that I will bear arms on behalf of the United States when required by the law; that I will perform noncombatant service in the Armed Forces of the United States when required by the law; that I will perform work of national importance under civilian direction when required by the law; and that I take this obligation freely without any mental reservation or purpose of evasion; so help me God.

    Sasa tafsiri, kama unajua ki-Ingereza, halafu uone kama nilipotosha chochote.

    ReplyDelete
  13. it doen't matter bado wanaruhusu dual citizenship kwa nchi fulani. don't be lazy just google and you will find all the information.

    ReplyDelete
  14. Wewe Mzushi Mbele hacha kupotosha,Hapa swala sio njinsi Mtazania anavyo kula-kiapo kuchukuwa urai wa nchi nyengine. SWALA ni njinsi ya kufanikisha Sisi Watanzania kuwa na Urai Pacha.Hatutakuwa inchi ya kwanza ya kiafrica kuwa na Urai Pacha including with USA. Mfano wa nchi za Africa zenye Urai pacha na USA ni Ghana,Benin,Togo,Lesotho,
    Namibia,Naigeria,Burkina Faso,Moroco,na kwa East Africa ni KENYA,huo ni Mfano tu!!!. Zipo nchi yingi Duniani zenye Urai pacha na USA,na hazijawahi kuwa matatani eti kwasababu zina urai pacha na USA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...