Jumuiya ya Watanzania Northampton UK imestushwa sana na taarifa ya ajali mbaya ya Meli ya abiria na mizigo iliyotokea jana usiku ikiwa safarini kuelekea Pemba. 

Sisi wanajumuiya tumeguswa sana na msiba huu na tupo pamoja nanyi katika wakati huu mgumu kwa wafiwa wote na wale walionusurika na ajali hiyo.

Tunaamini kabisa kuwa chanzo cha ajali hiyo kitachunguzwa na idara zinazohusika mara moja na taarifa zitatolewa katika vyombo vya habari.

MUHIMU zaidi ni idara husika kuzipitia upya taratibu zote zilizokwishawekwa na kuangalia ni wapi penye ‘gap’ katika taratibu hizo na hivyo kuhakisha utekelezaji wa taratibu zitazowekwa zinafuatwa na wahusika ngazi zote ili kuhakikisha maafa kama haya hayatokei tena. 

Na si vyombo vya majini tu, bali usalama katika barabara, reli, anga na waendao kwa miguu.

Mungu awaweke peponi marehemu wote na awape ujasiri wale wote walionusurika ili wapate nafuu mapema.

KNY Jumuiya,
William Maseke,
Katibu Jumuiya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...