Jumuia ya watanzania wa Uflipino (TSAP) kwa masikitiko makubwa tumepokea habari za msiba mkubwa ulioikumba nchi yetu katika ajali ya Meli ya Spice Islander huko Nungwi Zanzibar. 

Tunatoa salamu za rambirambi kwa watanzania wote ndugu jamaa na marafiki katika ajali hiyo. Ingawa tuko mbali lakini tuko pamoja nanyi katika msiba huu. 

Pia tunawaombea majeruhi wote wapone haraka na kuungana na ndugu na jamaa zao.
Tunaungana na ndugu zetu katika kipindi hiki kigumu na kuwatakia faraja na amani.

Vyuo vyote vyenye bendera zimepepea nusu mlingoti ili kuungana na wenzetu huko nyumbani katika msiba huu.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Africa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. mjomab wewe wa ufilipino tuwekee basi mawasiliano yenu huko ili sisi tukifika huko tujuwe wapi pa kuanzia na namna ya kuwatafuta watanzania wenzetu huko...

    ReplyDelete
  2. Naona bendera yetu imegeuzwa tena, dah!

    ReplyDelete
  3. Bendera yetu jamani kijani inakaa juu na bluu inatakiwa iwe chini!

    ReplyDelete
  4. sikujua ukiweka bendera nusu mligoti pia unaigeuza juu chini!!! Duh labda alikua anasisitiza.......

    ReplyDelete
  5. tunashukuru kwa maoni wadau! Tunaomba radhi kwa hiyo staili ya bendera ila tatizo ni kwamba chuo hubadilisha hizo bendera mara zinapokuwa chakavu na sometime hawatujulishi tunaona tu kitu kipya bila kuangalia imekaaje. Tunakiri ni makosa ya kutokuwa na tabia ya kufuatilia vitu kwa undani. Kwa kweli ni aibu kwetu ukichukulia hapa ni mahali panapofahamika sana. Tulisha rekebisha siku ile ile mdau wakwanza alipotukosoa.

    "Yes we learned through a mistake!"


    Asanteni wadau

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...