Jumuia ya watanzania wa Ufilipino (TSAP) kwa masikitiko makubwa tumepokea habari za msiba mkubwa ulioikumba nchi yetu katika ajali ya Meli ya Spice Islander huko Nungwi Zanzibar. Tunatoa salamu za rambirambi kwa watanzania wote ndugu jamaa na marafiki katika ajali hiyo. Ingawa tuko mbali lakini tuko pamoja nanyi katika msiba huu. Pia tunawaombea majeruhi wote wapone haraka na kuungana na ndugu na jamaa zao.
Tunaungana na ndugu zetu katika kipindi hiki kigumu na kuwatakia faraja na amani .
Vyuo vyote vyenye bendera zitapepea nusu mlingoti mpaka siku ya jumanne ili kuungana na wenzetu huko nyumbani katika msiba huu
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Africa
Asante.
MEDIA AND COMMUNICATION (TSAP)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...