Asalaam Aleykum,
Sisi ndugu zenu wa Leeds Swahili Community ya hapa Leeds U. K. Kwa mstuko mkubwa tumelazimika kupokea na kukubali taarifa yenye simanzi kubwa ya kuzama kwa meli ya Spice Islander iliyosababisha mamia ya ndugu zetu kupoteza maisha yao. Aidha wengine wengi kujeruhiwa. Hakika ni kipindi kigumu sana kwa wote walioguswa na tukio hili.
Hivyo basi Leeds Swahili Community inawapa POLE na kuwaombea SUBRA kwa majonzi haya mazito ya kihistoria. 
Hakika, Allah ni mkamilifu na mwingi wa rehma na kwa utukufu wake, Inshaallah atujaze nyoyo za imani na subra ili tuwe wastahamilivu na wenye kumshukuru kwa kila jambo. Allah tujaalie utulivu, umoja, upendo na ushirikiano hasa katika kipindi hiki cha majonzi.
AMEEN !
 
INNA LILAHII - WAINNA ILLAIHI  RAJIUNII
Asalaam Aleykum !
 
Amran Rashid
Mwenyekiti - Leeds Swahili Community 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...