Mwakilishi wa Umoja wa Afrika (African Union) Balozi Amina Salum Ali kwa niaba ya Umoja wa Afrika nchini Marekani, anaungana na Watanzania wote popote duniani, kuomboleza kutokana na maafa ya Watanzania wenzetu yaliyosababishwa na kuzama kwa meli ya Spice Islanders katika mkondo wa Nungwi, Kaskazini mwa kisiwa cha Unguja. Aidha, Balozi Amina Salum Ali anawapa pole wale wote waliofikwa na msiba huu mkubwa na kumwomba Mungu awafariji wale wote waliofikwa na tukio hili la kusikitisha.
Mwenyezi Mungu andelee kuwapa unafuu wa kiafya wale waliojeruhiwa katika tukio hili na pia azilaze roho za wale wote waliopoteza maisha yao mahali pema peponi, Amina.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...