Assalam Allaykum
Kwa niaba ya Wanafunzi wa Tanzania wote wanaoishi Malaysia .Tumeshitushwa sana na habari za tukio hili na tunaungana pamoja katika kuomboleza mtihani mkubwa huu uliotokea tareh 10/9/2011 wa kuzama kwa meli ya The MV Spice Islander na kusababisha vifo vya ndugu zetu . Katika hili hakuna wa kushukuriwa na kuombwa ila Mwenyezi Mungu kwa kuwapa uhai ndugu zetu na kuwarudisha mbele ya hali kwa wakati aliowapangia.
Msiba huu umetutia simanzi kubwa sana na tunamuomba M/Mungu atupe subra na atuzidishi umoja katika kuomboleza tulio hili la msiba a Taifa.
Tunatoa salam kwa viongozi wetu tulioataja hapo chini na ndugu zetu wote huko nyumbani.
1. Mhe Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohammed Shein,
2. Mhe Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na
3. Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Balozi Seif Ali Iddi.
Tunaungana na ndugu zetu kuomboleza na kutia fat-ha kwa msiba huu mkubwa sana uliotutokea.
Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi Aamin
Makame Hj Mohamed
Kuala Lumpur
Malaysia
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...