WATANZANIA tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kuzama kwa meli ya MV. Spice Islander katika pwani ya Nungwi na kuua ndugu zetu wapatao 200. Huu ni msiba mkubwa kwa taifa letu.
Mjengwablog, kama chombo cha jamii cha habari na mawasiliano kinatoa salamu za rambirambi kwa wahanga wote wa msiba huu mkubwa. Na tunachukua fursa hii kumpa mkono wa pole Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vivyo hivyo, mkono wetu wa pole umfikie Mheshimiwa Dr. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Ya Zanzibar.
Mjengwablog inaungana na Watanzania wote katika siku hizi tatu za maombelezo kwa kutorusha habari na picha za matukio yenye kuashiria sherehe na burudani.
Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania.
Maggid Mjengwa
Iringa,
11, Septemba, 2011
http://mjengwa.blogspot.com
http://mjengwa.blogspot.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...