Uongozi wa jumuia ya wanafunzi wa kitanzania wasomao nchini Algeria, kwa niaba ya wanajumuia wote tunapenda kuchukua fursa hii kufikisha Rambirambi zetu za dhati kwa watanzania wote kwa ujumla kufuatia ajali ya meli iliyotokea hivi karibuni.
Kwa kauli moja,wanafunzi wote wa kitanzania nchini Algeria Tunapenda kufikisha Rambirambi zetu za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Serikali Ya Mapinduzi Zanzibar DK. Ali Mohamed Shein kufuatia Msiba mkubwa uliolikumba Taifa letu baada ya kuzama kwa Meli ya Spices Islanders na kupoteza maisha ya mamia ya Ndugu,Jamaa na Marafiki tuwapendao ambapo wengine wamejeruhiwa na wengine wengi hawajulikani walipo.
Pia tunatoa salamu zetu za rambirambi kwa Ndugu,Jamaa na Marafiki wote walioguswa mojakwamoja na msiba huu na tunaomba mwenyezimungu awape moyo wa imani na ujasiri kwenye kipindi hiki kigumu cha mpito.Vilevile salamu za Rambirambi za wanafunzi wote wa kitanzania wasomao nchini Algeria kwa wanajumuia wote(wanaATSA) ambao kwa namna moja au nyingine wameguswa na Tukio hili,tunapenda kuwaambia kuwa tunaungana nao na tuko pamoja nao na Taifa kwa Ujumla kwenye kipindi hiki cha mpito,kuwafariji na kushirikiana nao kwenye kipindi hiki kigumu.
Tunapenda kuwakumbusha kuwa ‘’kila nafsi itaonja umauti na Bwana ametoa nae Bwana ametwaa, pia heshima pekee anayostahili marehemu ni kuzikwa na kuombewa dua(maombi) hivyo kwa pamoja tuungane tumuombe Mwenyezi Mungu aziweke Roho za Marehemu Mahala pema Peponi Aamin.
MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU TUBARIKI WATANZANIA ‘’
Kutoka kwa Uongozi,
THE ASSOCIATION OF TANZANIANS STUDENTS IN ALGERIA(ATSA)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...