INNA LILLAH WAINNA ILAIHI RA’AJIUN.
Uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jongowe na watu wa Jongowe wote kwa ujumla wanaungana na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Wazanzibari wote kutokana na msiba mkubwa uliyoikumba nchi kwa kuzama kwa meli ya Spice Islanders tarehe 10/09/2011.
Jumuia inatoa pole kwa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ndugu na jamaa wa wafiwa na wananchi wote kwa ujumla.
Aidha, Jumuia inawaomba ndugu, jamaa na familia zote zilizopatwa na msiba huu ziwe na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu waliotangulia mbele ya haki mahali pema peponi
Aaamin
Imetolewa na
Mohamed Ame Juma
Mkurugenzi Mtendaji
Mfuko wa Maendeleo ya Jongowe
Mkurugenzi Mtendaji
Mfuko wa Maendeleo ya Jongowe
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...