Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma ACP Fraisser Kashai (pili kushoto) pamoja na RCO wa mkoa huo,SSP Joseph Konyo wakiangakia Baiskeri zirizotumika kusafirishia risasi 2200 zikiwa nje ya kituo kikuu cha polisi cha kati mkoa huo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma ACP Fraisser Kashai akionyesha risasi zilizokamatwa.

NA P ardon Mbwate wa Jeshi la P olisi Kigoma

Jeshi la polisi mkoa wa kigoma limeendelea kufanya misako endelevu dhidi ya makosa mbalimbali ya jinai yakiwemo unyang’anyi wa kutumia silaha, wahamiaji haramu, madawa ya kulevya na makosa ya usalama barabarani. aidha mbinu mbalimbali zimetumika katika kuleta mafanikio ikiwemo doria, kufanya misako mbalimbali na vizuizi vya barabarani. mafanikio yaliyopatikana ni kama ifuatavyo :-

SEPT 10 2011 Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma ACP Fraisser Kashai, amesema kuwa jeshi la polisi limefanikiwa kukamata Risasi 2200 mnamo tarehe 07/09/2011 majira ya saa 01:00hrs huko uvinza katika wilaya na mkoa wa kigoma. askari polisi wakiwa kazini katika kizuizi cha barabarani (beria) waliwasimamisha watu watano waliokuwa na baiskeli kila mmoja kwa nia ya kuwapekua baada ya kuwatilia mashaka.

Kamanda Kashai amesema kuwa baada ya kuwatilia muda waliokuwa wakisafiri kwa baiskeli ghafla watu hao baada ya kugundua kuwa walikuwa wamesimamishwa na askari walitupa baiskeli zao na kukimbia huku wakizitelekeza baiskeli zao. vifurushi vilivyokuwa katika baiskeli hizo vilipekuliwa na zilipatikana risasi 2200 za bunduki za kivita aina ya S.M.G. / S.A.R.

Aidha Kamanda amesema kuwa Polisi waligundua risasi hizo zilikuwa zikisafirishwa kwa nia ya kufanyia vitendo vya uhalifu ndani na nje ya mkoa wa kigoma. jeshi la polisi linaendelea na msako mkali dhidi ya watuhumiwa hao waliotoroka.

Aidha Kamanda amesema jumla ya tshs 740,000/= zilikusanywa kama faini za makosa mbalimbali ya usalama barabarani yaliyokamatwa katika operesheni maalumu iliyofanyika kati ya tarehe 08/09/2011 na 09/09/2011.

Hata hivyo Kamanda Kashai amesema kuwaJeshi Jeshi la polisi linatoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano katika kufanikisha vita ya kupambana na uhalifu na wahalifu

Sanjari na hilo madereva na wamiliki wa vyombo vya usafiri wanatakiwa kufuata sheria na kuhakikisha magari yao yako katika viwango vya kubeba abiria kwa mujibu wa sheria na kwa mara nyingine ninawaimiza madereva wote ambao reseni zao zimekwisha muda wake kwenda kwenye mamlaka husika na kupata leseni hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Duh, hizo zote ziliandaliwa ili zikafanyie uhalifu.

    ReplyDelete
  2. Baiskeli za kivita

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...