
Miaka sita iliyopita,Muhidini Issa Michuzi kwa kufuata ushauri wa muasisi wa blogs za Kiswahili mtandaoni,Ndesanjo Macha,alianzisha kitu ambacho miaka sita baadaye kimekua kwa kasi na kiwango cha kipekee.Leo hii hakuna ubishi kwamba linapokuja suala la kublog,jina la Michuzi linachukuliwa kama “muongozo”.Blog ya Tanzania hivi leo ina uhusiano wa karibu na jina la Michuzi.Hayo ni mafanikio ambayo mtu yeyote anayeyabeza basi lazima awe aidha ana tatizo binafsi na Michuzi au kaamua tu kutoshughulisha akili yake kuhusu maendeleo ya ulimwengu wa mawasiliano na kupashana habari.
Naomba niungane na wengine wote katika kukupongeza Brother Michuzi (Ankal) kwa mafanikio hayo.Tafadhali endelea kuwaunganisha watanzania popote walipo ulimwenguni kupitia blog yako.Hongera,Hongera,Hongera!!
Niliwahi kufanya mahojiano kadhaa na Issa Michuzi.Lakini kwa kusoma mahojiano yangu naye kuhusiana na masuala ya blogs,tafadhali bonyeza hapa kuyasoma. Kusoma alichokiandika Michuzi kuhusu siku hii katika blog yake,bonyeza hapa.
Pichani juu ni Issa Michuzi akiwa na Ndesanjo Macha siku alipoingia rasmi katika ulimwengu wa kublog.
Kupata Chanzo BOFYA HAPA


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...