Watanzania tunaoishi katika jiji la Atlanta na vitongoji vyake tumeshtushwa, tumehuzunika na tumesikitishwa mno na taarifa za ajali ya meli ya Spice Islander iliyotokea September 10 2011.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu awalaze peponi wale wote waliofariki na tunawaombea wafiwa subra katika kipindi hiki kigumu.

Tunawashukuru sana wale wote waliofanya kazi ya kuokoa maisha na kusaidia kwa namna moja ama nyingine katika janga hili.

Halikadhalika, tunamshukuru sana Rais Jakaya Kikwete kwa kukatisha safari yake ya nje ya nchi kwa ajili ya kushughulikia janga hili. Pia tunamshukuru Dr. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kuwa mstari wa mbele katika kuwafariji wafiwa.

Kwa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais Wa Zanzibar Maalim Seif, Makamu wa Pili wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na viongozi wengine wa Zanzibar, Inshallah mwenyezi Mungu atawasaidia katika kuukabili mtihani huu.

Inna Lillahi wa Inna Ilaihi Raajiun.

Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.

John Kazilo

Rais wa Jumuiya ya Watanzania Waishio Atlanta

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...