Uongozi na wadau wote wa 'gazeti' mtandao la THEHABARI.COM unaungana na Watanzania wote katika maombolezo ya ajali na msiba mkubwa uliotokea Zanzibar, baada ya kuzama kwa Meli ya Mv. Spice Islander juzi usiku.

Thehabari imepokea kwa masikitiko makubwa na inawaombea majeruhi wote wa ajali hiyo wapone haraka ili warudi kuendelea na shughuli mbambali za ujenzi wa taifa. 
 
Kwa wafiwa tunawaombea kwa Mungu wapate nguvu katika kipindi hiki kigumu kwao na taifa. 
 
Mungu awapokee na kusamehewa dhabi zao ili baadaye waingie katika ufalme wa mbingu. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.

Imetolewa na Mhariri Mkuu wa Thehabari Tanzania, Joachim E. Mushi
www.thehabari.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA WATANZANIA WOTE KUTOKA WWW.TULONGE.COM

    Si rahisi kueleza uchungu mkubwa tulionao wana Tulonge juu ya ajali ya meli iliyotokea huko Zanzibar na kusababisha ndugu zetu kupoteza maisha.

    Kwa niaba ya Wadau wa Tulonge napenda kuungana na Watanzania wote katika maombolezo ya msiba huu mkubwa uliotukuta. Salamu za rambirambi ziwafikie wote waliopoteza ndugu zao na watanzania wote. Pia tunawapa pole wale waliyo nusurika katika ajali hiyo kwa msukosuko mkubwa walioupata katika kufanya jitahada za kuokoa maisha yao, wazidi kumshukuru Mungu kwa kuwanusuru.

    Mungu azidi kuwatia nguvu na moyo wa uvumilivu wale wote waliopoteza ndugu zao.

    Mwenyezi Mungu awalaze pema peponi wote waliopoteza maisha.

    Dismas Hiza,
    Mwenyekiti,
    www.tulonge.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...