Usiku wa Jumamosi tarehe 10 Septemba, 2011 kulitokea hitilafu ya kiufundi ya umeme katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere hali iliyosababisha kuvurugika kwa ratiba za ndege kadhaa ambazo wakati huo zilipaswa kuruka au kutua katika kiwanja hicho
Kutokana na hitilafu hiyo baadhi ya ndege zililazimika kuahirisha safari zao kwa kushindwa kuruka na nyingine ziililazimika kutua katika viwanja vingine vya jirani kama vile Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro, Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Zanzibar na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Jomo Kenyatta nchini Kenya.
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege inapenda kutoa ufafanuzi wa kuhusu chanzo cha tatizo hilo na hatua zilizochukuliwa kama ifuatavyo:
Chanzo cha tatizo hilo la kiufundi ni kushindwa kufanyakazi kwa mfumo wa mitambo unaotenganisha umeme unaofuliwa na jenereta za dharula kuruhusu matumizi ya umeme wa TANESCO. Hali hii ilipelekea kiwanja kuendelea kutumia jenereta za dharula hadi tatizo hilo liliporekebishwa asubuhi ya jumapili tarehe 11/09/2011 kwa ushirikiano wa wataalam wa TAA na TANESCO.
Wakati kukiwa na tatizo hilo katika mfumo wa mitambo ya kutenganisha matumizi ya umeme kulijitokeza hitilafu nyingine ya kuzimika kwa taa katika njia ya kurukia na kutua ndege na hivyo kushindikana kwa ndege kutua au kuruka kwa kipindi chote hicho.
Kufuatia hali hiyo wahandisi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege waliweza kufanya matengenezo ya mfumo huo wa umeme na Mnamo saa 7.30 usiku wa manane wataalam hao waliweza kufanikiwa kurudisha umeme kiwanjani hapo na kufanya baadhi ya ndege kuruka na kutua. Matengenezo kamili ya mfumo huo yalikamilika siku ya Jumapili, tarehe 11 Septemba, 2011. Kwa sasa shughuli za uendeshaji kiwanjani hapo zimeendelea kama kawaida.
Kikundi kazi cha wataalam kimeshaundwa kufanyia kazi suala hilo kwa undani zaidi kwa lengo la kupata kiini cha tatizo hilo, kufanya tahmini ya athari ziliopatikana na pia kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hilo kwa lengo la kuhakikisha kwamba halijitokezi tena.
Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania inasikitika sana kwa usumbufu na hasara zilitokana na tatizo hilo na tunawaomba radhi wateja wetu wote , hususani mashirika ya ndege, abiria, wadau wote na wananchi kwa ujumla.
Mwisho tunapenda kuwahakikishia kuwa hitilafu hiyo ya umeme ambayo kwa bahati mbaya ilitokea kiwanjani hapo usiku huo wa kuamkia tarehe 11 Septemba, 2011 halina uhusiano wowote na tishio la kigaidi kama ambavyo baadhi ya watu walihusisha tatizo hilo na lile lililotokea nchini Marekani tarehe 11 Septemba, 2001. Tunawahakikishieni kuwa kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere kina ulinzi wa kutosha kuthibiti matukio kama hayo ya kigaidi.
Mhandisi. Suleiman S. Suleiman
KAIMU MKURUGENZI MKUU
GOOD JOB MHANDISI SULEIMAN, INABIDI WATU WENGINE WAIGE MFANO WAKO KUHUSU COMMUNICATION. IMETOKEA ISHU, UMETOA MAELEZO YANAYOELEWEKA...IKIWEMO KUOMBA MSAMAHA, KUTAFUTA KIINI NA KUHAKIKISHA KUWA HAITATOKEA TENA
ReplyDeleteWacheni usanii wenu wa kibongobongo. Hivi leo siku ya tano ndiyo munatoa maelezo mulikuwa wapi siku zote hizo?
ReplyDeleteHalafu mumewacha mpaka ndege zimetaka kutua na kubidi kubadilisha ratiba munajua mumeingiza hasara kiasi gani kwa mashirika haya? Mbona tunachukulia mambo kienyeji enyeji kama vile lilivyokuwa marehemu shirika letu la ndege?
Mumefikiria angalau kuwalipa fidia hao waliopoteza muda wao hapo uwanjani na halafu ndege hazikutokea kutokana na kutowajibika kwenu?
HALAFU TUNATARAJIA UCHUMI UTAKUWA KWA MAASILIMIA KIBAO KWA MWAKA, LABDA UCHUMI HUU WA WANYWAJI BIA UTAKUWA BAADA YA KARNE MOJA.
Blaa!blaa!blaa! Kama kawaida yenu hamkosi la kusema. Tanzania sekta zote kwa sasa ni uozo mtupu. Nilitua na KLM mwaka jana KIA nilikua naelekea Daa. Ndege ilipokua inataka kupaa kuelekea daa rubani kasema naomba samahani nizime taa za ndani kwani sioni njia vizuri baadhi ya taa zimezima. Nilipata sana uchungu nikijua ni dola maelfu wanalipa kutua kwa nusu saa tu uwanjani pale. Hata pesa ya taa midomoni mwa mafisadi. Mkiambiwa muachie nchi wengine nao wajaribishe hamtaki. Shame on you all wahusika wala msiombe msamaha subirini tu siku ndugu zake Osama watawaamsha.
ReplyDeleteMdau USA
hii hali iliniboa sana, mlniharibia mipango yangu, muwe makini sio kuomba radhi KILA SIKU
ReplyDeleteAaagh, kichefuchefu, too many excuses!
ReplyDeleteBongo kila siku ni aibu tupu wahusika hawafai kabisa kiwanja kawaida kiwe na jenereta special lipo tayari wakati wowote ule, Tutafika kweli namna hii jamani kila kkukicha Bongo ni kicheko kwa watu.
ReplyDeletetunalishwa mavi kwa kinywaji mkojo.
ReplyDeletenihayo tu niliyonayo.
mtanzania.
Mie nilikuwa mmojawapo wa abiria ambaye nilitakiwa kusafiri na ndege ya KLM toka Dar hadi Amsterdam na baadae niunganishe na ndege ya kwenda Detroit. Nilipocheck-in tu, nkasikia abiria wa Swiss International wanataarifiwa hwataweza kusafiri, watapelekwa mahotelini. Check-in ikaendelea kwa sie wa KLM na precision ambayo ilikua iende Johannesburg. Umeme uliokuwepo ni wa jenereta, uliweza kuwasha taa tu, na tena si zote. Ndani ya nyumba ya kusubiria ndege kulikuwa na joto ajabu. Ndege yetu ilikuwa tupande saa 4 na dk 55 usiku. Tukatangaziwa tutapewa taarifa baada ya nusu saa. Wakakaa kimya hadi saa 7 unusu usiku. Abiria wakaanza kulalama, ndio tangazo la KLM (watanzania hawa waliopo eapoti) likatoka ndege haitakuwepo hadi kesho yake saa 3 usiku. Hawa walijua hatutasafiri lakini waliendelea kukaa kimya hadi usiku wa manane. Walishajua marubani walifika Kilimanjaro, wakasubiri hadi saa 5, wakaamua kwenda kulala. Ya nini walituweka eapoti muda wote. Tumepelekwa kulala Dabo Tree, Southern Sun, Movenpick pamoja na New Africa hotel. Mabasi yametuchukua sote saa 11 na nusu jioni kesho yake. Hii ilisababisha foleni kubwa jabu ya kucheck-in. Muda huu huu Precision ya Johanessburg ikawa inacheck-in pia. Na wale regular abiria wa KLM wa siku hiyo wakaanza kucheck in. Jamani nilimsikia mama mmoja mmatumbi anasema anaukana utanzania wake maana tunatia aibu. Amani tunayo lakini ni kwa sababu tunavumilia maumivu.
ReplyDeleteCheck in ilikua slow ajabu.
Tumepanda ndege na tumefika salama Amsterdam. Kuna interview za security kwa wale abiria wanaoenda marekani. Jamani, ile kujulikana tu natokea Tanzania na KLM. Yule askari swali la kwanza, vipi umeme wa barabara za ndege unawezaje kukatika? Ina maana walipokea taarifa tayari. Na delay ya ndege yetu ilijulikana Amsterdam na kuleta gumzo. Mie nilikosa jibu la msingi, nikamwambia Tanzania ina power rationing.
Kinachoumiza, Swiss walidivert ndege ikaenda kutua kwa watani zetu, wao wako serious.
All in all, ni aibu kubwa sana.
GOOD JOB MHANDISI SULEIMAN!!!? KILO WEWE NI MNAFIKI FISADI. UMETUMWA LAZIMA, ACHA KUTETEA UJINGA! AU NDIO MHUSIKA MWENYEWE NINI? POOR YOU.
ReplyDeleteNi aibu tupu then mnaleta maelezo ujinga hapa.Hii ndo "tumeweza" theme ya miaka 50,upuuzi hawa watu waanaachwa wangewajibishwa hamna mtu angeleta upuuzi.Matatizo tunakubali huwa yanatokea ila hatua za haraka za utatuzi kuepusha yote haya ndo mlichotakuwa kufanya.
ReplyDeleteMIMI PIA NILIKUA MMOJA WA ABIRIA WA KLM, NILILAZIMIKA KURUDI NYUMBANI.....NI UZEMBE! INTERNATIONAL AIRPORT KAMA HII NA MIJIHELA MNAYOKUSANYA MLITAKIWA MUWE MNA MULTIPLE BACK UP PLANS..sio kutegemea system moja tu ya umeme.
ReplyDeleteTBC Walitangaza siku hiyo??? Naomba maelezo
ReplyDeletesuleiman s. suleiman jina hilo jibu tafuta mwenywe. nd'o maana meli zinajaza kupita kiasi. watu, mizigo, nahodha hajui chombo kina uzito gani, watu wana uzito gani, mizigo ina uzito gani. mambo ya kienyeji sana. mtadai hata marekani umeme ulikatika na ndege hazikutua. lakini ni nature ilisabibisha hayo siyo hii ya kwetu. WAJIBIKA MZEE SSS UKAONGOZE SIMBA.
ReplyDeleteyani hii nchi imeoza ni takataka pumbav kabisa, hela zinakusanywa nyingi tuu hapo airport ila vitu vya muhimu kuweka sawa ni tatizo, inamaana wanashindwa kununua standby generators likitokea la kutokea zinajiwasha na mambo yanaendelea? alafu mnaiita international airport? hata ngazi za umeme kupanda hapo juu kwenda kusubiri ku-board ndege ni mbovu, mtu unapanga foleni kwenda kuchek in hilo joto hapo hakuna hata ac, hivi hii nchi ina laana au ni nini? michuzi bania na hii km kawaida yako
ReplyDeleteWote mliochangia hapo juu mmeshalishwa kasumba. Nafikiri wengi wenu mmesoma maelezo lakini hamkuyaelewa ama kwa makusudi au kutokana na jazba mlizo nazo. Matatizo yameelezwa vizuri na tujiuliza tangu nyie mmepata akili ya kwenda nchi za watu huko ni mara ngapi tatizo hili limetokea pale JKNA? sio mnalalama kama vile hata hizo nchi zinazoendelea uwa hazitokei dharura kama hizo.
ReplyDeleteWakati mwingine tunatakiwa tujiamini na kile tunachojua na si kuponda tu.
hizi nchi za watu hakuna upuuzi km huu wewe uliecomment hapo juu, ushasikia hata hapo kenya tuu wala tusiende mbali kuna siku umeme ulikatika kwenye airport? unajua ni kiasi gani hizi ndege/kampuni zao zinalipa kutua kwenye huo uwanja wenu unaotetea? acha ujinga wewe ni bora ukae kimya
ReplyDelete