Mwanadada ambaye jina lake halikuweza fahamika mara moja mkazi wa maeneo ya Mtaa wa Gofu,jijini Tanga akiosha vyombo vyake pembeni ya reli huku vingine akiwa kaviweka ndani ya reli hiyo ambayo haitumiki kwa kipindi kirefu sasa.huku mahindi yakiwa yamestawi kiasi cha kupendezesha eneo hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. kitu gani kinawafanya watu watake kuishi mahali kama hapo. na kwanini wapaharibu hapo. hiyo reli ikifufuliwa watakwenda wapi. na ni kwanini waachiwe kuaribu mazingira ya hiyo sehemu. wahusika shuhulikieni hiyo sehemu. michuzi keep them coming kwasababu picha kama hizi ni za kuwaamsha wqhusika. hivi hawa watu hukagua sehemu zao au wanakaa ofisini peke yake. please wake up.

    ReplyDelete
  2. Hii ndiyo bongo bwana, wabongo ni wataalamu wa mipango mizuri nadhani kuliko nchi yoyote duniani, tatizo ni utekelezaji na sustainability. Hiyo reli ukiuliza ilijengwa lini utaaambiwa toka ukoloni.Sasa hapo tunalalamika nini?

    ReplyDelete
  3. Wahusika sio kama hawajui lakini kwasababu hawatapata kipato hapo inakuwa sio muhimu kwao.Wahusika huchangamkia suala ambalo linakajiposho fulani.Halafu hao watu ukiwatoa hapo hujifanya kudai haki zao na kujiweka kama wameonewa wakati mtu na akili zake timamu hawezi kaa ktk eneo ambalo haliruhusiwi na kwa faida ya wote.Chukueni mfano wa KENYA sehemu iliyotokea moto ni sehemu imetengwa kwa ajili ya viwanda na ni kwa manufaa ya wananchi wenyewe,lakini watu ndio wamekwenda kujenga karibu na mapaipu ya mafuta ambayo inahatarisha maisha yao na afya zao kwa kukaa karibu na viwanda.Na tumeona jinsi madhara yaliyotokea na wangapi wamepoteza maisha.Serikali inatakiwa iwadhibiti watu kabla ya ujenzi kwasababu wakishajenga labda watu 200 inakuwa tabu sana kuwatoa maana wanataka serikali iwalipe fidia kutokana na kuwahamisha.Kwanini hawasaidii kuwapatia viwanja sehemu zinazotakiwa na ujenzi ukae kwa mpangilio sio shaghalabaghala hata ikitokea dharura gari la kuzima moto au la wagonjwa haliwezi pita huko.Yaani serikali na wananchi hatuna system nzuri ya mpangilio na kuondoa huu umaskini tuna upa kipaumbele wenyewe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...