Na Ripota wa Globu ya Jamii, Bagamoyo

BENDI muziki wa dansi nchini ya Twanga Pepeta 'wazee wa kisigino' imefanya shoo kali usiku wa kuamkia leo katika uzinduzi wa tamasha la 30 la sanaa na utamaduni wa chuo cha Bagamoyo.

Katika shoo hiyo ya aina yake, Twanga iliweza kutikisa vilivyo na kuamsha shangwe na vifijo kwa mashabiki waliofurika ukumbini huko hasa pale walipopiga nyimbo zao mpya na zile za zamani ndani ya ukumbi huo wa TaSUBa hali iliyowainua mashabiki kwenda jukwaani kuselebuka.

Miongoni mwa waliotia fora katika uzinduzi wa tamasha hilo ni wanenguaji wote wa bendi hiyo,pamoja na muimbaji wa siku nyingi Muumin Mwijuma 'mtoto wa Bagamoyo' ambaye aliimba kwa hisia kali akisaidiana na mkongwe mwenzake Ruiza Mbutu na wengineo kwa vibao hivyo vipya na vya zamani.

Awali kabla ya Twanga kutumbuiza vikundi mbalimbali vya ngoma na sanaa kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani vilitumbuiza ukumbini hapo huku umati mkubwa ukiwa umefurika kushuhudia maonyesho hayo wakiwemo wageni wa ndani na nje.

Tamasha hilo la sanaa la 30 limeanza Juzi na linataraji kuisha Octoba Mosi mwaka huu na litafungwa na Waziri wa Habari,Utamaduni,Vijana na Michezo, Dkt. Emmanuel Nchimbi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...