MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam , Said Meck Sadik akizungumza na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi wakati uongozi wa Mkoa huo ulipofika ofisini kwa makamu huyo kumpa pole kufuatia kutokea kwa ajali ya kuzama kwa meli ya Mv. Spice islander sambamba na hilo uongozi huo pia ulichangia shilingi milioni 60 ikiwa ni msaada kwa waathirika wa ajali hiyo.
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadik akimkabidhi Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hundi ya mfano ya shilingi milioni 60 ikiwa ni msaada uliotolewa na wananchi wa Dar es salaam kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa ajali ya Mv Spice islander , mkuu huyo alifika ofisini kwa makamu huyo akiwa na viongozi wengine wa mkoa huo wakiwemo wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama wa mkoa huo na viongozi wa kisiasa.
MWENYEKITI wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Sylevester Massele Mabumba (kushoto) akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 20 Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi , zilizotolewa na Bunge hilo kwa ajili ya kusaidia waathirika wa ajali ya Mv. Spice islander , makabidhiano hayo yalifanyika ofisini kwa Makamu huyo iliyopo Vuga mjini Unguja jana.
MWENYEKITI wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Sylevester Massele Mabumba (kushoto) akizungumza na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kabla ya kumkabidhi msaada wa shilingi milioni 20 zilizotolewa na Bunge hilo kusaidia waathirika wa ajali ya Meli ya Mv. Spice islander, mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa makamu huyo Vuga mjini Unguja jana.
MWENYEKITI wa Makampuni ya Arabian Night Hoteli na Swahili Beach Resort, Noushad Mohammed (kushoto) akimkabidhi Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, msaada wa shilingi milioni 17 ikiwa ni kwa ajili ya waathirika wa ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv. Spice islander 1. Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za makamu huyo Vuga mjini Unguja jana.
MAKAMU wa pili wa Rais wa Zanzibar , Balozi Seif Ali Iddi (kulia) akipokea hundi ya shilingi milioni tano kutoka kwa muakilishi wa kampuni ya Meli ya Mv. Flying Horse, Khamis Said ikiwa ni msaada kwa waathirika wa ajali ya kuzama kwa meli ya Mv. Spice islander 1 makabidhiano hayo yalifanyika ofisini kwa Makamu huyo Vuga mjini Unguja jana. ( Picha na Haroub Hussein) .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...