Miti ya Michikichiki ikiwa imeanguka chini kutokana na uchimbaji wa mchanga uliokuwa ukifanyika katika kijiji cha Nkema,mkoani Kigoma.
baadhi ya maeneo ya mashamba ya Michikichi yaliyoharibiwa vibaya kutokana na uchimbaji huo wa mchanga.
Baadhi ya wakazi wa Buronge wakiwa katika hali ya Simanzi kutokana vifo vya watoto hao.
Mti wa Mwembe ukiwa umekauka kutokana kufukuliwa mizizi yake na wachimaji wa mchanga.
Na Pardon Mbwate, wa Jeshi la Polisi Kigoma
KIGOMA IJUMAA, SEPTEMBA 23,2011. Wanafunzi wawili wa shule ya msingi Buronge mjini Kigoma,wamefariki dunia baada ya roli walilokuwa wamepanda kuangukiwa na kifusi kilichokuwa kimerundikana kwenye machimbo ya udongo wakati wanafunzi hao wakitoka machimboni hapo.
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma ACP Fraisser Kashai, amewataja wanafunzi hao kuwa ni Mussa Ibrahimu(16) na Yusuph Ismai(16), wote ni wanafunzi wa darasa la sita katika shule hiyo.
Kamanda Kashai amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya Saa 12 jioni jana huko kwenye eneo la Nkema mjini Kigoma na miili ya marehemu hao ilifukuliwa na kukabidhiwa kwa ndugu zao kwa shughuli za mazishi.
Kamanda kashai ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha kuwa watoto waliopo chini ya umri wa miaka 18 wanazingatia masomo na kuacha kufanya kazi za kujipatia kipato zikiwemo hizo za uchimbaji mchanga ambazo ni hatari kwa maisha yao.
Amesema shughuli kama hizo pia zinapunguza maendeleo ya mtoto shuleni na ni kinyume cha sheria na haki za mtoto.
Katika maeneo ya Nkema kuna uharibifu mkubwa wa mazingira kutokana na shughuli za uchimbaji udongo unaotumika kwa kujengea nyumba mjini humo na ameziomba mamlaka husika kuchukua hatua dhidi ya wale wote wanaoharibu mazingira kwa kisingizio cha kujitafutia kipato.


CCM Oyeeee?? Oyeeeee !
ReplyDeleteKikwete Oyeee?? Oyeeee !!!
Michuzi Blog Oyeee??? Oyeeee
Watanzania Wote Oyeeee??? Oyeeee!!
Hahaha haaaa
Chimba chimba Oyeee!!!
Mdau wa Kilosa
yote hiyo ni kutokana na umaskini,utakuta hao watoto ndio wanaolisha familia zao,mungu azilaze roho za marehemu mahali pepa peponi Amin.
ReplyDeletesasa hapo panachimbwa mpaka panafikia hivyo ndo leo wanastuka na kwenda na vikamera vyao ???? hapo hapajachimbwa siku moja , kamata wote mwenyekiti wa serikali , mjumbe, diwani wote ndani ....pambaff
ReplyDelete