Wawakilishi toka Benki ya Dunia na Washiriki wa Maendeleo wakisiliza kwa makini mjadala wa Warsha ya Wadau wa Hifadhi ya Mazingira ya Ziwa Victoria (LVEMP 11)  inayofanyika katika Hotel  ya Imperial  Botanical  Beach Resort hapa Entebe Uganda. Wadau wa Maendeleo wamesisitiza umuhimu wa kuendelea na  Hifandhi ya Maizingira na Utekelezaji wa miradi  mbalimbali katika Ziwa hilo.
 Mkurugenzi Msaidizi  anayeshughulikia Maji shirikishi (Transboundary Waters) katika Wizara ya Maji  Injinia Sylvester Matemu akitoa mada katika Warsha hiyo.Kulia Kwake ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Rasilimali za Maji katika Wizara ya Maji Injinia Naomi Lupimo.
 Mtaalamu wa Benki ya Dunia anayeshughukilia  Mawasiliano kanda ya Afrika Mashariki  Bwana Steven Shalita  akitoa maoni yake katika majadiliano na Wadau mabalimbali kwenye Warsha hiyo.Mwenye miwani kushoto ni Mratibu wa Mradi wa Hifadhi ya Mazingira ya Ziwa Victoria (LVEMP 11)  kwa upande wa Tanzania Injinia Pius Mabuba.
Imperial Botanical Beach Hotel hapa Entebe amabako Warsha hiyo inafanyika.

Na Nurdin Ndimbe

Warsha ya Kimataifa ya Wadau wa Hifadhi ya Mazingira ya Ziwa Victoria inaendelea hapa Entebe Uganda kwa lengo la kutathimini maendeleo ya mradi huo ikihusisha Wadau, Makatibu Wakuu wa Wizara zinazohusika na Mradi huo toka Nchi za Afrika Masharki na pamoja na Wahisani wa Maendeleo wakiwemo Benki ya Dunia.

Washiriki wa Warsha wameomba watekelezaji wa Mradi sasa kuwa na nia ya dhati kabisa ya kuona kuwa maendeleo ya Miradi mabalimbali inakuwa endelevu kwa manufaa ya Wananchi wa Nchi hizo.

Hata hivyo Wadau wengi waliiomba Benki ya Dunia kupunguza urasimu katika masula yote yanayohusu Fedha na Manunuzi kwani, kwa maoni yao Miradi mingi inachelewa kuanza kwa sababu hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...