Ubalozi wa Tanzania Kuala Lumpur, Malaysia ulifungua kitabu cha maombolezi (condolences book) kuwaombea wahanga wa ajali ya Meli "MV Spice Islanders" iliyotokea Visiwa vya Zanzibar usiku wa kuamkia tarehe 10 September 2011. 

Wawikilishi toka Serikali ya Malaysia na Jumuiya ya Kibalozi walijitokeza na kutoa salamu za pole kwa Serikali na WANANCHI wa Watanzania kufuatia msiba huo mkubwa. Aidha, wawakilishi wa Makampuni yenye mahusiano ya kibiashara na Tanzania pia walifika kwa ajili hiyo. Jumuiya ya Watanzania waishio Malaysia iliwakilishwa na Dr. Kassim A. Abdullah (Eng.) Mkufunzi Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Malaysia (International Islamic University of Malaysia - IIUM), ambacho kina idadi kubwa ya watanzania toka Visiwani.

Wakati huo huo, Jumuiya ya Watanzania iliandaa Dua Maalum katika Chuo Kikuu IIUM kuwarehemu wote waliopoteza maisha katika ajali ya "MV Spice Islanders" Watanzania walijitokeza kwa wingi toka majimbo kadhaa nchini Malaysia na kushiriki katika maombi hayo maalum yaliyofanyika baada ya Sala ya Ijumaa tarehe 16 Septemba 2011. Ubalozi wa Tanzania uliwakilishwa na Kaimu Balozi Bw. Simba Yahya, ambaye kwa niaba ya Ubalozi, alifikisha salamu za pole kwa wanajumuia walioathirika moja kwa moja, na kwa watanzania kwa ujumla kwa kupoteleza idadi kubwa ya maisha ya Watanzania katika ajili hiyo.

Mungu Awaweke Wote Mahala Pema Peponi.
Mungu Ibariki Tanzania. AMEEN.
Balozi wa China akitia sini kitabu cha maombolezo.
Wawikilishi toka Serikali ya Malaysia akitoa pole kwa Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Malaysia,Bw. Simba Yahya.
Balozi wa Afrika ya Kusini.
Balozi wa Sudan.
Balozi wa Canada.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. jamani hawa sio wahanga, hawakujitolea kufa hawa ni waathirika , msitupotoshe ohoo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...